Tusker
ya Kenya, imekuwa timu ya kwanza kufuzu Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi,
baada ya jioni hii kuilaza Jamhuri ya Pemba bao 1-0, lililofungwa na
mshambuliaji wake hatari, Jesse Were dakika ya 23 kwenye Uwanja wa Amaan,
Zanzibar. Mabingwa hao wa Kenya, sasa wamefikisha pointi saba na kujiimarisha
kileleni mwa Kundi A na kwa matokeo hayo, Simba SC pia tayari imefuzu Nusu
Fainali, kwani mabingwa hao wa Bara tayari wana pointi nne hadi sasa, wakati
Jamhuri imemaliza na tatu na Bandari haina pointi hata moja. Simba inacheza
mechi ya mwisho na Bandari usiku Amaan.
source: Bin Zubeiry
on Sunday, January 6, 2013
Post a Comment