“Kuwa na maadui ili kukupa vyote sio lazima, lakini ni
vizuri. Hasa pale unapokuwa unafurahia mafanikio na unajisahau na
kujiachia." Jose Mourinho
Jose Mourinho anaweza akawa
amepigilia msumari wa mwisho kwenye jeneza lake. Uamuzi wa kumuacha Iker
Casillas, nahodha wa klabu, mchezaji ambaye ndio nembo inayowakilisha Real
Madrid, uamuzi huo wa Mourinho unatafsiriwa kuwa jaribio la kujiua mwenye
kwa “Special one”.
Katika hii vita inayoendelea ya madaraka
pale Bernabeau, Mourinho ameenda mbali kwenye suala hili Casillas. Raisi
Florentino Perez amekuwa hafurahishwi na tabia za Mourinho na ripoti zinasema
kwamba yeye yupo upande wa Casillas katika vita inayoendelea dhidi ya
Mou.
MCHEZO
WA MOURINHO:
Tangu alipowasili pale Madrid Mourinho ameweza kuiongoza timu
yake kwa njia moja tu anayoijua yeye, utata. Imani yake ni kwamba inabidi
atafute namna yakucheza na saikolojia za wapinzani wake au 'maadui' ili
kufanikiwa.
Ilikuwa ni sababu hii ambayo iliwafanya Barcelona wakatae
kumpa ajira ya kuwa kocha wao mwaka 2008. Mfumo wake wa uendeshaji timu
ulilpelekea watu kuchukiana na kugombana.
Perez alimleta Madrid kuja
kuondoa utawala wa Barcelona kwenye La Liga. Hasira zake dhidi ya Barcelona
ambao walimchagua Guardiola badala yake ziliongoza hisia zake. Matamanio yake ya
kuwatukana kisaikolojia wakatalunya na maneja wao yaliongozwa na mambo yake
binafsi dhidi ya Barca. Ilionekana kuwa zaidi ya 'mind games', hii ilikuwa hatua
ya utashi wake binafsi kuiharibia klabu ambayo ndio imekuwa nembo ya utamu wa
soka.
Je
Perez aliuza roho ya klabu kwa shetani?
Ingawa muongo uliopita umekuwa
m'baya na usio na mafanikio kwa Real, lakini ufahari na asili ya Madrid siku
zote umekuwa ni wa kujiona kama 'Wafalme wa Soka'. Wachezaji kama Zidane,
Puskas, Di Stefano, Raul na Ronaldo De Lima wote wamewahi kuvaa uzi mweupe na
kuleta mafanikio na heshima kwa klabu hiyo.
Ujio wa Cristiano Ronaldo,
Benzema na Kaka ulikuwa unaaminisha ni kuundwa kwa 'Galatico' mpya. Mourinho
alionekana ndio mwanaume anayefaa kuipeleka timu kwenye kilele cha mafanikio
tena. Na msimu uliopita Mourinho alifanikiwa kuwa bingwa wa La Liga na jinsi
mashabiki walivyoshangilia ilionyesha ni kiasi gani ubingwa huo ulikuwa na
umuhimu kwa klabu, wachezaji na wapenzi wa Madrid. Madrid walikuwa hawazuiliki
mwaka uliopita, wakizishinda timu kwa spidi yao kali, nguvu na viwango bora vya
wachezaji. Lakini walishindwa kufanikiwa barani ulaya, wakishindwa kuleta
ubingwa wa 10 wa Ulaya ambao mashabiki na Raisi wa timu hiyo wanauota kila
siku.
Ukweli
ni kwamba Perez alikuwa tayari kumpa kila Mourinho kama ilikuwa ni kwa ajili ya
kushinda. Huu ni mchezo hatari kuucheza na matokeo yake yanaonekana sasa.
Mourinho alitaka kuwa na mamlaka ya kila kitu; usajili, soka la vijana, na
mipango mengine yanayohusu kikosi chake. Kama ilivyo kwa makocha wachache kwenye
ulimwengu wa soka, alitaka kupewa mamalka makubwa ndani ya
klabu.
Ingawa Jorge Valdano aliondolewa kwa sababu hakuwa
akikubaliana na Mourinho na sera zake, haikuwa rahisi kwa Mourinho. Perez
anaonekana kupoteza uatayari wako wa kumkabidhi Mourinho madaraka yote na
wachezaji wa muda mrefu wa kihispania wanaonekana kutokuwa na furaha na
kinachoendelea. Vita kati ya kocha na wachezaji (kitu ambacho cha kawaida kwenye
klabu yake ya zamani ya Chelsea) ni kitu kinachoendelea na Perez anaonekana
kuwepo upande wa wachezaji dhidi ya kocha wao.
Mourinho alitaka
kuibadilisha Madrid na sera yao na alitaka kupata madaraka ya kuipeleka timu
mbele zaidi. Lakini anaona matamanio yake ya kuibadilisha klabu hayakubaliki na
hayaaminiki. Mourinho hivyo anaamua kushindana na wanaompinga, tabia ambayo
inaweza ikawa na matokeo mabaya kwa matamanio yake ya kutaka kushinda kombe la
Ulaya akiwa na timu ya 3 tofauti.
Je Mourinho hakuielewa
Madrid?
Sera yenye kuongozwa na utata inaweza kuwa ilifanikiwa katika
vilabu vyake vya nyuma huko kama vile Inter na Chelsea, ilileta mafanikio na
mashabiki na wachezaji walimpenda na kumtukuzakwa hilo. Ingawa, kosa lake kwa
wakati huu ni kuamini Real Madrid itakuwa ni kama klabu zake alizofundisha
nyuma.
Pale Inter, Chelsea na Porto Mourinho alikuwa mshindi na
alipendwa na wachezaji na mashabiki. Alizipeleka timu zake kutawala ligi za
nyumbani na ulaya akiwa na Porto na Inter. Yalikuwa ni mafanikio kwa kocha huyo
mreno na hakuna la kushangaza Madrid wakaamua kumchukua. Ingawa, mafanikio
katika zile klabu huko nyuma yalikuja kutokana na sera yake ya kucheza na
saikolojia za wachezaji wake, vyombo vya habari na wapinzani wake ilifanya
kazi.
Alivichukua vikosi ambavyo vilionekana na wengi kuwa vya kawaida na
kuvifanya kuwa mabingwa. Akaja Madrid ambapo ni klabu yenye utajiri wa utamaduni
na historia na yenye kujiamini yenyewe kama ndio klabu bora duniani; sio tu kwa
suala la mafanikio bali pia na staili. Mashabiki walitaka mafanikio na bado
wakataka kuona soka safi likitandazwa.
Wakati staili ya Barcelona ikiwa
inatajwa kuwa bora kama ilivyo kwa timu ya Spain, Madrid walikuwa wanaonekana wa
kawaida. Staili ya kidachi/kikatalunya ya kucheza soka iliwavutia mashabiki na
muhimu zaidi ikapelekea mafanikio makubwa katika historia ya
Barcelona.
Badala ya ya kuikumbatia staili hiyo, Mourinho akaamua kwenda
kinyume chake. Alitaka timu yake icheze kama Inter zamani, ilinde, icheze kibabe
ili kupunguza mashambulizi ya wachezaji hasa kwenye za El Classico. Aliwaambia
wachezaji wake wafanye udanganyifu, na kuwatisha Barcelona. Ingawa, kwa sababu
nyingi staili hii haikuweza kufanya kazi, Barca waliendelea kushinda na Mourinho
na Madrid walikuwa wanaonekana tu kama wagomvi, wenye wivu ya vipaji vya
mahasimu wao.
Ingawa wachezaji kama Pepe, Marcelo na Di Maria waliletwa
maalum kwa sera zaMourinho ya soka, kuna wachezaji ambao hawakuwa wanakubaliana
na sera zake za kucheza soka la kibabe, nje na ndani ya
uwanja.
Haikushangaza kwamba walikuwa ni Casillas, Ramos na Alonso ambao
walionyesha kutokukubaliana na kuucheza mchezo wa Mourinho. Wachezaji hawa ambao
walishinda kombe la dunia na Euro wakiwa na Spain hivyo walikuwa wanashea
mahusiano mazuri na wachezaji wa Barca. Mourinho sasa alikuwa akitaka kuwafanya
wachezaji hao wawaone Barca maadui zao na kuwaletea ubabe wenzao ambao ni
marafiki zao timu ya taifa ya nchi yao.
Akiwa na Inter na Chelsea
alifanikiwa kuwaaminisha wachezaji kufuata sera yake, muda huu sera yake hiyo
imekutana na upinzani mkali dhidi ya wachezaji wenye nguvu ndani ya
klabu.
Madrid msimu uliopita chini ya Mourinho walikuwa vizuri na moja ya
vilabu vya kuogopwa barani ulaya. Walikuwa na safu yenye makali mno iliyokuwa na
njaa ya kufanya balaa kwenye nyavu za wapinzani wao. Pointi zao na magoli
yalionyesha ni kiasi gani walitisha, na hatimaye waliweza kuwafunika
Barcelona.
Msimu huu mambo yamebadilika. Ule moto haupo tena, kile
kilichokuwa kinawapa motisha ya kutaka kushinda zaidi kinaonekana kimepotea.
Timu inaonekana kugawanyika, na klabu yote inaonekana kama jumba la sanaa za
maonyesho ya nani aliyebora miongoni mwao.
JE MOURINHO ANAMMISI MPINZANI
WAKE?
Mwanzoni mwa makala haya kulikuwepo na kauli iliyosema -
“Kuwa na
maadui ili kukupa vyote sio lazima, lakini ni vizuri. Hasa pale unapokuwa
unafurahia mafanikio na unajisahau na kujiachia."
Inaonekana sasa baada
ya kufanikiwa kushinda La Liga kikosi cha Madrid msimu kilikuwa kinalenga kwenye
Champions league, huku Guardiola akiwa ameondoka tayari na Madrid wakimuongeza
Luka Modric kwenye kikosi chao kilichokuwa boratayari, ilionekana hakuna
kitakachowasimamisha. Lakini mambo yamegeuka sasa hivi, wanauana wenyewe kwa
wenyewe sasa hivi. Suala la Guardiola kama mpinzani linaanza kuleta maana
sasa.
Mourinho alisema kwenye kauli yake hapo juu kuhusu Guardiola
kwamba mpinzani wake huyo alikuwa ni mtu ambaye alimfanya awe anafanya kazi kwa
juhuhdi sana. Inaonekana kwamba Mourinho alifanya kazi akimuangalia kama
Guardiola kama changamoto kwake na wachezaji wake.
Kuwashinda Barca na kocha
wao ikawa ni kitu ambacho kiliingia kwenye hisia za Mourinho kuwa ni lazima
hata iweje. Msimu uliopita alishinda, Guardiola alishindwa na Madrid
walishangilia sana. Lakini sasa Guardiola akiwa ameondoka, Madrid wamepoteza
hali ya kupigana ya msimu uliopit, Madrid wamekosa kitu cha kuwasukuma
kushindana zaidi? Adui yao mkubwa aliyewasumbua vilivyo ameondoka, amewaacha
Mourinho na Madrid yake wakiwa wana hisia za upweke.
Kwa mujibu wa
Mourinho alikuwa mpinzani wake aliyempa msukumo wa kushindana zaidi, hivyo
inawezekana kuondoka kwake kumemfanya ali-relax kama alivyosema, kitu ambacho
kinaonekana kimewaingia wachezaji na hivyo kuleta madhara kwenye
matokeo.
Mourinho sasa anaonekana ameshindwa kazi, wachezaji baadhi na
raisi wanaripotiwa kumchoka na kuna hisia zipo kwamba mabadiliko yanatakiwa
kwenye klabu.
Inaonekana mwisho wa Mourinho ndani ya Santiago Bernabeu
umewadia. Yeye mwenyewe, wachezaji, mashabiki na raisi kuna hisia zinazojieleza
wamefikia sehemu wote wanasema kauli moja 'Imetosha'. Kwa Mourinho atakuwa na
machaguo mengi baada ya Madrid, sehemu ambayo atakuwa analipwa £10million kwa
mwaka. Japokuwa, ikiwa ataondoka Madrid bila medali ya ushindi wa Champions
league, atakuwa amefeli katika kazi yake kubwa kabisa tangu aanze kufundisha
soka.
Jose Mourinho anaweza akawa amepigilia msumari wa mwisho kwenye jeneza lake. Uamuzi wa kumuacha Iker Casillas, nahodha wa klabu, mchezaji ambaye ndio nembo inayowakilisha Real Madrid, uamuzi huo wa Mourinho unatafsiriwa kuwa jaribio la kujiua mwenye kwa “Special one”.
Katika hii vita inayoendelea ya madaraka pale Bernabeau, Mourinho ameenda mbali kwenye suala hili Casillas. Raisi Florentino Perez amekuwa hafurahishwi na tabia za Mourinho na ripoti zinasema kwamba yeye yupo upande wa Casillas katika vita inayoendelea dhidi ya Mou.
Tangu alipowasili pale Madrid Mourinho ameweza kuiongoza timu yake kwa njia moja tu anayoijua yeye, utata. Imani yake ni kwamba inabidi atafute namna yakucheza na saikolojia za wapinzani wake au 'maadui' ili kufanikiwa.
Ilikuwa ni sababu hii ambayo iliwafanya Barcelona wakatae kumpa ajira ya kuwa kocha wao mwaka 2008. Mfumo wake wa uendeshaji timu ulilpelekea watu kuchukiana na kugombana.
Perez alimleta Madrid kuja kuondoa utawala wa Barcelona kwenye La Liga. Hasira zake dhidi ya Barcelona ambao walimchagua Guardiola badala yake ziliongoza hisia zake. Matamanio yake ya kuwatukana kisaikolojia wakatalunya na maneja wao yaliongozwa na mambo yake binafsi dhidi ya Barca. Ilionekana kuwa zaidi ya 'mind games', hii ilikuwa hatua ya utashi wake binafsi kuiharibia klabu ambayo ndio imekuwa nembo ya utamu wa soka.
Je
Perez aliuza roho ya klabu kwa shetani?
Ingawa muongo uliopita umekuwa m'baya na usio na mafanikio kwa Real, lakini ufahari na asili ya Madrid siku zote umekuwa ni wa kujiona kama 'Wafalme wa Soka'. Wachezaji kama Zidane, Puskas, Di Stefano, Raul na Ronaldo De Lima wote wamewahi kuvaa uzi mweupe na kuleta mafanikio na heshima kwa klabu hiyo.
Ujio wa Cristiano Ronaldo, Benzema na Kaka ulikuwa unaaminisha ni kuundwa kwa 'Galatico' mpya. Mourinho alionekana ndio mwanaume anayefaa kuipeleka timu kwenye kilele cha mafanikio tena. Na msimu uliopita Mourinho alifanikiwa kuwa bingwa wa La Liga na jinsi mashabiki walivyoshangilia ilionyesha ni kiasi gani ubingwa huo ulikuwa na umuhimu kwa klabu, wachezaji na wapenzi wa Madrid. Madrid walikuwa hawazuiliki mwaka uliopita, wakizishinda timu kwa spidi yao kali, nguvu na viwango bora vya wachezaji. Lakini walishindwa kufanikiwa barani ulaya, wakishindwa kuleta ubingwa wa 10 wa Ulaya ambao mashabiki na Raisi wa timu hiyo wanauota kila siku.
Ukweli
ni kwamba Perez alikuwa tayari kumpa kila Mourinho kama ilikuwa ni kwa ajili ya
kushinda. Huu ni mchezo hatari kuucheza na matokeo yake yanaonekana sasa.
Mourinho alitaka kuwa na mamlaka ya kila kitu; usajili, soka la vijana, na
mipango mengine yanayohusu kikosi chake. Kama ilivyo kwa makocha wachache kwenye
ulimwengu wa soka, alitaka kupewa mamalka makubwa ndani ya
klabu.Ingawa muongo uliopita umekuwa m'baya na usio na mafanikio kwa Real, lakini ufahari na asili ya Madrid siku zote umekuwa ni wa kujiona kama 'Wafalme wa Soka'. Wachezaji kama Zidane, Puskas, Di Stefano, Raul na Ronaldo De Lima wote wamewahi kuvaa uzi mweupe na kuleta mafanikio na heshima kwa klabu hiyo.
Ujio wa Cristiano Ronaldo, Benzema na Kaka ulikuwa unaaminisha ni kuundwa kwa 'Galatico' mpya. Mourinho alionekana ndio mwanaume anayefaa kuipeleka timu kwenye kilele cha mafanikio tena. Na msimu uliopita Mourinho alifanikiwa kuwa bingwa wa La Liga na jinsi mashabiki walivyoshangilia ilionyesha ni kiasi gani ubingwa huo ulikuwa na umuhimu kwa klabu, wachezaji na wapenzi wa Madrid. Madrid walikuwa hawazuiliki mwaka uliopita, wakizishinda timu kwa spidi yao kali, nguvu na viwango bora vya wachezaji. Lakini walishindwa kufanikiwa barani ulaya, wakishindwa kuleta ubingwa wa 10 wa Ulaya ambao mashabiki na Raisi wa timu hiyo wanauota kila siku.
Ingawa Jorge Valdano aliondolewa kwa sababu hakuwa akikubaliana na Mourinho na sera zake, haikuwa rahisi kwa Mourinho. Perez anaonekana kupoteza uatayari wako wa kumkabidhi Mourinho madaraka yote na wachezaji wa muda mrefu wa kihispania wanaonekana kutokuwa na furaha na kinachoendelea. Vita kati ya kocha na wachezaji (kitu ambacho cha kawaida kwenye klabu yake ya zamani ya Chelsea) ni kitu kinachoendelea na Perez anaonekana kuwepo upande wa wachezaji dhidi ya kocha wao.
Mourinho alitaka kuibadilisha Madrid na sera yao na alitaka kupata madaraka ya kuipeleka timu mbele zaidi. Lakini anaona matamanio yake ya kuibadilisha klabu hayakubaliki na hayaaminiki. Mourinho hivyo anaamua kushindana na wanaompinga, tabia ambayo inaweza ikawa na matokeo mabaya kwa matamanio yake ya kutaka kushinda kombe la Ulaya akiwa na timu ya 3 tofauti.
Je Mourinho hakuielewa Madrid?
Sera yenye kuongozwa na utata inaweza kuwa ilifanikiwa katika vilabu vyake vya nyuma huko kama vile Inter na Chelsea, ilileta mafanikio na mashabiki na wachezaji walimpenda na kumtukuzakwa hilo. Ingawa, kosa lake kwa wakati huu ni kuamini Real Madrid itakuwa ni kama klabu zake alizofundisha nyuma.
Pale Inter, Chelsea na Porto Mourinho alikuwa mshindi na alipendwa na wachezaji na mashabiki. Alizipeleka timu zake kutawala ligi za nyumbani na ulaya akiwa na Porto na Inter. Yalikuwa ni mafanikio kwa kocha huyo mreno na hakuna la kushangaza Madrid wakaamua kumchukua. Ingawa, mafanikio katika zile klabu huko nyuma yalikuja kutokana na sera yake ya kucheza na saikolojia za wachezaji wake, vyombo vya habari na wapinzani wake ilifanya kazi.
Alivichukua vikosi ambavyo vilionekana na wengi kuwa vya kawaida na kuvifanya kuwa mabingwa. Akaja Madrid ambapo ni klabu yenye utajiri wa utamaduni na historia na yenye kujiamini yenyewe kama ndio klabu bora duniani; sio tu kwa suala la mafanikio bali pia na staili. Mashabiki walitaka mafanikio na bado wakataka kuona soka safi likitandazwa.
Wakati staili ya Barcelona ikiwa inatajwa kuwa bora kama ilivyo kwa timu ya Spain, Madrid walikuwa wanaonekana wa kawaida. Staili ya kidachi/kikatalunya ya kucheza soka iliwavutia mashabiki na muhimu zaidi ikapelekea mafanikio makubwa katika historia ya Barcelona.
Badala ya ya kuikumbatia staili hiyo, Mourinho akaamua kwenda kinyume chake. Alitaka timu yake icheze kama Inter zamani, ilinde, icheze kibabe ili kupunguza mashambulizi ya wachezaji hasa kwenye za El Classico. Aliwaambia wachezaji wake wafanye udanganyifu, na kuwatisha Barcelona. Ingawa, kwa sababu nyingi staili hii haikuweza kufanya kazi, Barca waliendelea kushinda na Mourinho na Madrid walikuwa wanaonekana tu kama wagomvi, wenye wivu ya vipaji vya mahasimu wao.
Ingawa wachezaji kama Pepe, Marcelo na Di Maria waliletwa maalum kwa sera zaMourinho ya soka, kuna wachezaji ambao hawakuwa wanakubaliana na sera zake za kucheza soka la kibabe, nje na ndani ya uwanja.
Haikushangaza kwamba walikuwa ni Casillas, Ramos na Alonso ambao walionyesha kutokukubaliana na kuucheza mchezo wa Mourinho. Wachezaji hawa ambao walishinda kombe la dunia na Euro wakiwa na Spain hivyo walikuwa wanashea mahusiano mazuri na wachezaji wa Barca. Mourinho sasa alikuwa akitaka kuwafanya wachezaji hao wawaone Barca maadui zao na kuwaletea ubabe wenzao ambao ni marafiki zao timu ya taifa ya nchi yao.
Akiwa na Inter na Chelsea alifanikiwa kuwaaminisha wachezaji kufuata sera yake, muda huu sera yake hiyo imekutana na upinzani mkali dhidi ya wachezaji wenye nguvu ndani ya klabu.
Madrid msimu uliopita chini ya Mourinho walikuwa vizuri na moja ya vilabu vya kuogopwa barani ulaya. Walikuwa na safu yenye makali mno iliyokuwa na njaa ya kufanya balaa kwenye nyavu za wapinzani wao. Pointi zao na magoli yalionyesha ni kiasi gani walitisha, na hatimaye waliweza kuwafunika Barcelona.
Msimu huu mambo yamebadilika. Ule moto haupo tena, kile kilichokuwa kinawapa motisha ya kutaka kushinda zaidi kinaonekana kimepotea. Timu inaonekana kugawanyika, na klabu yote inaonekana kama jumba la sanaa za maonyesho ya nani aliyebora miongoni mwao.
JE MOURINHO ANAMMISI MPINZANI WAKE?
Mwanzoni mwa makala haya kulikuwepo na kauli iliyosema -
“Kuwa na maadui ili kukupa vyote sio lazima, lakini ni vizuri. Hasa pale unapokuwa unafurahia mafanikio na unajisahau na kujiachia."
Inaonekana sasa baada ya kufanikiwa kushinda La Liga kikosi cha Madrid msimu kilikuwa kinalenga kwenye Champions league, huku Guardiola akiwa ameondoka tayari na Madrid wakimuongeza Luka Modric kwenye kikosi chao kilichokuwa boratayari, ilionekana hakuna kitakachowasimamisha. Lakini mambo yamegeuka sasa hivi, wanauana wenyewe kwa wenyewe sasa hivi. Suala la Guardiola kama mpinzani linaanza kuleta maana sasa.
Mourinho alisema kwenye kauli yake hapo juu kuhusu Guardiola kwamba mpinzani wake huyo alikuwa ni mtu ambaye alimfanya awe anafanya kazi kwa juhuhdi sana. Inaonekana kwamba Mourinho alifanya kazi akimuangalia kama Guardiola kama changamoto kwake na wachezaji wake.
Kuwashinda Barca na kocha wao ikawa ni kitu ambacho kiliingia kwenye hisia za Mourinho kuwa ni lazima hata iweje. Msimu uliopita alishinda, Guardiola alishindwa na Madrid walishangilia sana. Lakini sasa Guardiola akiwa ameondoka, Madrid wamepoteza hali ya kupigana ya msimu uliopit, Madrid wamekosa kitu cha kuwasukuma kushindana zaidi? Adui yao mkubwa aliyewasumbua vilivyo ameondoka, amewaacha Mourinho na Madrid yake wakiwa wana hisia za upweke.
Kwa mujibu wa Mourinho alikuwa mpinzani wake aliyempa msukumo wa kushindana zaidi, hivyo inawezekana kuondoka kwake kumemfanya ali-relax kama alivyosema, kitu ambacho kinaonekana kimewaingia wachezaji na hivyo kuleta madhara kwenye matokeo.
Mourinho sasa anaonekana ameshindwa kazi, wachezaji baadhi na raisi wanaripotiwa kumchoka na kuna hisia zipo kwamba mabadiliko yanatakiwa kwenye klabu.
Inaonekana mwisho wa Mourinho ndani ya Santiago Bernabeu umewadia. Yeye mwenyewe, wachezaji, mashabiki na raisi kuna hisia zinazojieleza wamefikia sehemu wote wanasema kauli moja 'Imetosha'. Kwa Mourinho atakuwa na machaguo mengi baada ya Madrid, sehemu ambayo atakuwa analipwa £10million kwa mwaka. Japokuwa, ikiwa ataondoka Madrid bila medali ya ushindi wa Champions league, atakuwa amefeli katika kazi yake kubwa kabisa tangu aanze kufundisha soka.
Post a Comment