Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Wakulima wapigwa msasa



Na  Happiness Amos, Bunda -Mara

Asilima 80 ya wananchi wa bunda wanatengemea kilimo ,ufugaji na uvuvi anbapo hulima mazao mbalimbali ikiwemo mihogo,mtama,mahindi,pamba pamoja na zao la alzeti na meinge mengi

Akizungumza katika mafunzo ya klilimo bora cha alzeti,mpunga ,ufugaji wa kuku wa asili na samaki katika mabwawa na huduma za fedha vijijini katika ukumbi wa Serengeti resort wilayani bunda mkoani mara jana kaimu mkurugenzi bi DINNA RWEIMAMU amesema pamoja na hayo wanakabiriana na changamoto nyingi ikiwemo mabadiriko ya hali ya hewa

Bi Dinna amesema mbali na changamoto hiyo amezitaja changamoto zingine ikiwa ni wadudu waharibifu wa mazao,ubovu wa miundombinu,na ukosefu wa habari sahihi na mapema kwa mkulima hali inayopelekea kushuka kwa kiwango cha uzalishaji na upatikanaji wa mazao

Aidha katika mafunzo hayo yaliyoandaliwa na shirika lisilokuwa la kiserikali la third millennium initiative foundation {TMPIF} linaloendesha na mradi wa MDG Acceleration framework{MAF}ambalo linafadhiliwa na shirika la maendeleo la umoja wa mataifa {UNDP} ,bi Dinna amesema halmashauri ya wilaya imekuwa na mikakati mbalimbali ikiwemo kuhimiza kilimo cha umwagiliaji ,ujenzi wa majosho kuhimiza matumizi ya mbegu ya mazao ya kisasa pamoja kusimamia mpango wa serikali wa kutoa pembejeo
Naye mwezeshaji bwana Johanes A.Bucha akitoa maeelekezo juu ya kilimo cha zao la alzeti kwa wakulima na washiriki waliohudhuri mafunzo hayo amesema zao hilo likilimwa na kutuzwa vizuri humunufaisha mkulima kwani ekari moja hutoa kilo 1500-3000 ambapo kwa kukamua mafuta kilo 60-80 hutoa lita 18-25 kutegemeana na mbegu aliyoitumia mkulima
Akijibu swali la mshiriki wa mafunzo hayo aliyetaka kujua juu ya Shirika hilo la maf litawasaidiaje wananchi wanaotaka kufuga kuku wa asili Bi Violet mkama ambaye pia ni Afisa mradi huo amesema kuwa kwa mfugaji anayehitaji kusaidiwa na shirika hilo anatakiwa kuwa na dhamira na mwelekeo wa kuwa na banda na anatakiwa kuwa na kuku angalau 30
Bi Mkama amesema watakuwa na mashine itakayokuwa inatotoresha vifaranga ambapo mashine hiyo itakuwa na uwezo wa kutotoresha vifaranga 1100 kwa siku 18 na vifaranga hivyo vitagawiwa kwa wafugaji na pamoja na kupewa jogoo moja lenye uwezo wa kuzalisha majike 20
Shirika la TMPIF linaloshuhulika na masuala mtambuka ambayo ni kilimo bora cha zao la alzeti,mbunga,ufugaji wa kuku wa asili , ufugaji wa samaki kwenye mabwawa na huduma za fedha vijijini linalengo la kutokomeza umaskini kwa kutoa elimu kwa wakulima pia linashirikiana na halmashauri ya wilaya ya bunda
Hata hivyo mkurugenzi wa MAF Respice mkama amewaomba washiriki kupeana changamoto zilizopo ili waweze kufika mbali katika kuendeleza mradi na mradi huo umeongezwa mwaka mmoja ili kuweza kuendelea kutoa huduma hali itakayosaidia zaidi kutokomeza umasikini
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top