Na Bryceson Mathias,
Mvomero
WANANCHI wa mji mdogo wa Mvomero wamemtaka Waziri
wa Maji Prof. Jumanne Maghembe (pichani) aende katika mji huo akajionee madudu ya mradi
wa maji wa zaidi ya Bilioni mbili unavyochezewa, huku wao wanapata shida ya
maji.
Kauli hiyo ilitolewa
Januari 15, 2013 na wakazi wa Mji huo waliokuwa mto Mvomero na mwandishi
kuwahoji kwa nini wanaoga, kufua na kuchota maji hayo hayo kwa ajili ya
matumizi ya nyumbani, ambapo walidai madudu na kero ya Mradi wao wa maji
umewafikisha hapo.
Wakizungumza kwa nyakati
tofauti, wanaume na wanaume waliokuwa wakitoka kuoga, kufua na kuchota maji kwa
ajili ya matumizi ya nyumbani walisema, kwa hali ya shida ya maji safi ambayo
wakazi wa mvoero tumefikia, tunamtaka Waziri wa Maji Prof. Maghembe aje ajionee
madudu ya mradi wao wa maji wa Bilioni mbili unavyochezewa, ilihali wao
wanapata shida.
“Mradi huu ulianza Januari
2012 na ulitakiwa ukabidhiwe mwaka jana June 6, 2012, lakini sasa umesimama na
haujulikanai utaishi lini ndiyo maana tunalazimika kuoga, kufua na kuchota maji
ya kunywa hapa hapa. Je mwandishi unadhani twenda wapi?”.
Mwanamke mmoja Mama
Lishe kwa niaba ya wenzake alisema, Baba; Mimi ni Mama Nitiliye kama
unavyoniona, kama naona Mitambo imelala haifanyi kazi, unanitaka niamini na
kujidanganya kuwa maji yatakuja wakati hayapo? Ukitaka maji ya visima vya watu,
lazima ununue!.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi
na Sekondari Mvomero waliozungumza na mwandishi kama nao wanapata shida ya maji
walikiri na kusema, mara kadhaa wakiwauliza viongozi wa Kata wanawaambia kuwa,
Mkandarasi amesimama kufanya kazi kutokana na kutolipwa kwa wakati, na pia
wanadai aliongezewa Mkata hadi Januari mwaaka huu lakini hatuoni, hapa kuna
ujanja.
Aidha Mwandishi
alimtafuta Diwani wa Kata ya Mji Mdogo wa Mvomero Selemani Mwinyi (CCM) alikiri
Mradi kusimama na kuwepo kwa Kampuni ya Kichina ya CCECC ambayo imeshafanya
kazi Asilimia 88% na kulipwa takribani Milioni 600/-, na pia alieleza ipo
Kampuni ya Ushauri ya Kimisri ya AAA-Consulting Engineer yenye Mhandisi.
“Hata mimi nashangaa
Mradi kwa nini hauishi licha ya kuongezewa muda. Malipo kwa wakandarasi
yanachelewa, vyombo vimesimama, kazi haifanyiki, hivyo hata mimi sijui kama
fedha hiyo ipo au kuna mchezo mchafu sielewi!! Naungana na wananchi Waziri aje
awapatie majibu”. alisema Diwani Mwinyi baada ya kubanwa.
Post a Comment