Rais
Jakaya Mrisho Kikwete
Na
Kambi Mbwana, Dar es Salaam
HALI
inazidi kuwa mbaya kwa vurugu na maandamano, baada ya wasanii kutangaza kufanya
maandamano mfululizo, endapo Serikali itaendelea kuchekea dhuluma na manyanyaso
wanayoendelea kufanyiwa wasanii hapa nchini.
Michael
Sangu, Mwenyekiti TDFAA
Hatari
hiyo ilitangazwa jana na wasanii zaidi ya 200 waliokutana katika Ukumbi wa
Vijana, Kinondoni, wakiongozwa na viongozi wao kutoka Mashirikisho mbalimbali,
ikiwamo lile la Filamu TAFF.
Simon
Mwapagata, msanii wa filamu Tanzania
Handeni
Kwetu ilikuwapo katika viwanja hivyo na kukuta wasanii wengi waliokuwa
wakijadili mambo yao huku wakiwa na hasira kali kutoka kwa viongozi, hasa wale
wa COSOTA na Bodi ya Filamu Tanzania, chini ya Mkurugenzi wake, Joyce
Fisoo.
Akizungumza
na Handeni Kwetu, Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji Tanzania (TDFAA), Michael
Sangu, alisema sheria zilizotungwa kwa ajili ya wasanii hazina
mashiko.
Alisema
sheria hizo zitazidi kuongeza maisha duni kwa wasanii Tanzania, kama walivyokufa
baadhi yao wakiwa hawana chochote cha maana zaidi ya kufanikiwa kuwa
maarufu.
“Mchakato
mzima wa kanuni za utekelezaji wa sheria ya filamu na michezo ya kuigiza
Tanzania Bara haukuhusisha wasanii wadau, wakiwamo wasanii.
“Hii
ni hatari maana itaongeza ugumu wa utendaji kazi, huku wachache wao kuendelea
kufanikiwa, huku serikali ikiwa kimya, jambo ambalo kwa pamoja hatiwezi
kulichekea,” alisema.
Awali
wasanii wengi walipata kutoa maoni yao katika kutafuta maisha bora ya wasanii,
huku lawama zao zote wakizielekeza kwa watendaji wa juu wa COSOTA, chini ya
Yustus Mkinga na Joyce Fisoo wakitaka waondoshwe katika nafasi zao.
“Kama
hakutakuwa na mabadiliko katika nafasi za watu hawa, hakika hatuwezi kufanya nao
kazi, maana kauli zao, matendo yao katika suala zima la sanaa hatuna imani
nayo,” alisema Simon Mwapagata akiungwa mkono na mamia ya wasanii
wenzake.
Endapo
wasanii hao watafanya maandamano bila kuchoka kushinikiza watendaji hao wang’oke
katika nafasi zao, ni wazi nao watakuwa wameingia katika kutingisha utawala wa
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, mmoja wa viongozi wa juu wan chi wanaokubaliwa na
waliokuwa karibu mno na wasanii hapa nchini.
Serikali
kwa kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo inapaswa kuliangalia
hilo kwa haraka kabla ya kuzidi kuingiza chokochoko katika vuguvu vugu hizo za
wasanii kwa kusikiliza kilio cha wasanii wao.
Post a Comment