Sajuki
enzi za uhai wake akiwa na mke wake, kipenzi chake, Wastara
Na
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WADAU
wa sanaa hapa nchini, wameendelea kummwagia sifa mwanadada Wastara Juma,
aliyekuwa mke wa marehemu Sadiki Juma Kilowoko, maarufu kama Sajuki kuwa ana
moyo wa aina yake.
Hiyo
imetokana na historia ya uhusiano wake na Sajuki hadi kufunga ndoa kukumbwa na
mitihan mingi, jambo ambaloh hivyo halikumfanya ajiweke kando na
Sajuki.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, kwa tiketi ya Chadema, Zitto Kabwe, alisema kwamba Wastara ana mapenzi ya dhati na anastahili sifa.
Alisema
ameweza kumuuguza mumewe mwanzo hadi mwisho wa uhai wake, jambo ambalo limekuwa
gumu kwa baadhi ya watu, kadri muda unavyozidi kwenda mbele.
"Ni
mfano wa kuigwa kwakweli kutokana na historia na matatizo mengi yaliyowakumba
yeye na mumewe hadi kufariki na kuzikwa Ijumaa katika makaburi ya Kisutu,"
alisema.
Naye
Mbunge wa Kinondoni, kwa tiketi ya (CCM), Idd Azzan, alisema amekuwa karibu na
sanaa kiasi cha kumuona Wastara ni miongoni mwa wanawake makini.
"Kwa
dunia ya leo kumuuguza mume wako katika kipindi kigumu cha ugonjwa wake, hadi
kuchangiwa fedha za kumpeleka India, hakika baadhi yao wanaweza kuleta wasiwasi
kidogo,” alisema Azzan.
Azzan
ni miongoni mwa wabunge wanaofuatilia sanaa kwa karibu zaidi, huku wasanii wengi
wakikimbilia kwake kila wanapokuwa na jambo linalohusu msaada kutoka kwa jamii
nzima.



Post a Comment