|
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Celina
Ompeshi Kombani akizungumza mapema leo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa
Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi Tanzania katika
ukumbi wa Benki Kuu Mwanza. |
|
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Celina
Kombani amewapongeza wakaguzi hao kwa kuboresha usimamizi wa mapato na
matumizi ya mali ya Umma, kwani matunda ya kazi za Ofisi ya Taifa ya
Ukaguzi yameijengea nchi ya Tanzania sifa nzuri siyo tu kwa raia wa
Tanzania, bali mbele ya wadau wote wanaotakia mema nchi hii. |
|
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo kwa upande wake amelia na baadhi ya
watendaji waliotajwa katika Taarifa ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG)
kutafuna fedha za Umma huku wakiendelea na kazi bila hatua za kisheria
kuchukuliwa dhidi yao, ameitaka serikali kulitizama hilo kwa jicho la
tatu na kuchukua hatua za haraka kusafisha waliobakizwa. |
|
Mkutano
huu unatajwa kuwa ni wa pili kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2012/2013,
Madhumuni yake ni kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Ofisi ya Taifa
ya Ukaguzi. |
|
Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Ndugu ludovick S.L Utouh
akimtambulisha Mkurugenzi wa jiji la mwanza Bw. Wilson Kabwe, wakati wa
ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya
Ukaguzi Tanzania katika ukumbi wa Benki Kuu Mwanza. |
|
Wakaguzi hao walipata fursa ya kuimba wimbo wa mshikamano kwa wafanyakazi. |
|
Meza kuu nayo ilihusika na wimbo huo wa mshikamano. |
|
Katika
kuboresha mazingira ya kufanyia kazi na kupunguza suala la Ofisi ya
Wakaguzi kutegemea Ofisi za Wakaguliwa jitihada zimeanza kufanyika na
mpaka sasa Ofisi imeweza kujenga Ofisi zake katika mikoa ya manyara,
Shinyanga, Singida, Mbeya, Lindi, Kilimanjaro na Morogoro aidha Ofisi
ilinunua jengo na kulifanyia ukarabati mkoani Arusha. |
|
Mshikamano na Wakaguzi waliohudhuria mkutano wao wa Mwaka katika ukumbi wa Benki Kuu Mwanza. |
|
Moja
kati ya Changamoto ambazo Afisi ya Mkaguzi wa fedha za Serikali bado
inaendelea kukumbana nazo ni Idadi ndogo ya rasilimali watu
ukilinganisha na ongezeko la ofisi kupitia Mikoa mipya, Halmashauri za
wilaya mpya na ukaguzi wa Umoja wa Mataifa. |
|
Picha namba moja. |
on Tuesday, January 22, 2013
Post a Comment