Waziri mkuu Mizengo Pinda akipokewa na viongozi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu mara baada ya kuwasili katika ofisi hiyo kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na Ofisi hiyo jijini Dar es salaam.
Waziri mkuu Mizengo Pinda akipata maelezo kuhusu
matumizi ya ramani katika upataji na ukusanyaji wa takwimu mbalimbali
zinazotumiwa katika masuala mbalimbali nchini kutoka kwa Kaimu Meneja wa Idara
ya Mbinu za Kitakwimu, Viwango na Uratibu Bw. Emilian
Karugendo.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt.
Albina Chuwa (kulia)akimfafanulia jambo Waziri Mkuu Mizengo Pinda
(katikati) kuhusu takwimu za Kilimo na uchumi. Kushoto kwa waziri Mkuu ni
Waziri wa Fedha Dkt. William Mgimwa.
Waziri mkuu Mizengo pinda (kulia katikati) akitazama
takwimu mbalimbali alipotembelea kitengo cha ramani akiwa na Waziri wa Fedha na
Uchumi Dkt. William Mgimwa (kushoto), Dkt. Albina Chuwa Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi
ya Taifa ya Takwimu (kulia).
Mkuu wa Kitengo cha Ramani Ofisi ya Taifa ya Takwimu
Vincent Mgaya (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda
kuhusu matumizi ya ramani kupata Takwimu za Kilimo, Uchumi
na Utalii.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimweleza jambo Meneja wa
Takwimu za Kilimo Bi. Joyce Urassa alipotembelea Ofisi ya Taifa ya Takwimu
jijini Dar es salaam.
Meneja wa Idara ya Pato la Taifa wa Ofisi ya Taifa ya
Takwimu Bw. Daniel Mwasula akitoa ufafanuzi kwa Waziri mkuu Mizengo Pinda kuhusu
Pato la Taifa na namna ofisi yao inavyofanya kazi kukokotoa pato la
taifa.
Post a Comment