Waziri Simba akiangalia
baadhi ya vyerehani viwili viliyotolewa na Lions kwa ajili ya kuwasaidia
wanawake wajane. Vyerehani hivyo ni kati ya 100 vitakavyotolewa na Lions
kuwawezesha wanawake kujikimu kimaisha.
*****
Na Usu-Emma Sindila na
Sakina Mfinanga
Waziri wa Maendeleo ya
Jamii,Jinsia na Watoto Mhe.Sophia Simba amekabidhi msaada wa vyerehani viwili
kati ya 100 vilivyotolewa kwa wanawake wajane wa Mkoa wa Dar es Salaam
ofisini kwake leo kutoka Taasisi ya Lions Club.
Akizungumza kwenye hafla
fupi ya kukabidhi vyerehani hivyo, Gavana wa Lions Ukanda wa Tanzania na
Uganda, Ndg. Joseph Kiwanuka, amesema taasisi yao imekuwa mstari wa mbele
kuisaidia jamii hasa wanawake na watoto, kuboresha huduma za maji kwa kuchimba
visima ambavyo huwasaidia wananchi hasa wanaokaa sehemu zenye shida ya
maji.
Amesema Lions imekuwa
ikisaidia watoto wenye matatizo ya moyo kuwapeleka nchini India kwa ajili ya
matibabu,kuwasaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu kwa kuwapeleka
shule hasa zile za awali na wameanzisha mkakati wa kuwaelimisha wanafunzi
mashuleni kuhusu utumiaji wa madawa ya kulevya ili watoto wasijihusishe na
vitendo hivyo.
Kwa upande wake Waziri
Simba ameishukuru taasisi ya Lions kwa misaada mbalimbali ambayo wamekuwa
wakiisaidia jamii na zaidi kwa msaada huo wa vyerehani kwa wajane kwa kuwa
utawawezesha kujikwamua kimaisha wao wenyewe, watoto na familia
zao.
Aidha, Waziri Simba
amewapongeza Lions kwa kazi kubwa wanayofanya kupitia mradi wao wa kuelimisha
wanafunzi juu ya madhara ya utumiaji wa dawa za kulevya na kuongeza kuwa
Serikali inafanya jitihada kuhakikisha kila kata inakuwa na shule ili kusaidia
kupunguza wimbi la watoto wasiojua kusoma na kuandika
Post a Comment