Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa akikata utepe wa
uzinduzi wa maabara ya kisasa iliyogharimu milioni 49 ikiwa ni sehemu ya mradi
wa vijiji vya Milenia wa Mbola jana wilayani Uyui wakati Waziri huyo
alipotembelea Wilaya hiyo kuona mradi wa mfano ulivyoboresha maisha ya wananchi
katika vijiji 16 zinavyoteleza mradi huo. Kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Uyui Said Shaban Ntahondi na kushoto ni Mbunge wa Jimbo Tabora Kaskazini Mamlo
Shafin Sumar na wapili kutoka kushoto ni Kiongozi wa Mradi wa Vijiji vya Milenia
wa Mbola Dkt Gerson Nyadzi.
Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa(kushoto) akiongea na
viongozi wa vijiji 16 vinavyotekeleza mradi wa vijiji vya Milenia wa Mbola
jana wilayani Uyui juu ya kuufanya mradi huo kuwa darasa endelevu kwa ajili ya
vijiji vingine nchini kwenda kujifunza juu ya utekeleza wa malengo 8 ya Milenia
. Waziri huyo alitembelea Wilaya hiyo kuona mradi wa mfano ulivyoboresha maisha
ya wananchi katika vijiji 16 zinavyoteleza mradi huo. Katikati ni Mwnyekiti wa
Halmashauri ya Uyui Said Shaban Ntahondi na kulia ni Mwenyekiti wa Kijiji cha
Ilolangulu Ally Magoha.
Waziri
wa Fedha Dkt William Mgimwa amewataka wakazi wa Wilaya ya Uyui mkoani Tabora
waliopo katika wa utekelezaji malengo ya Milenia chini ya mradi wa vijiji vya
Milenia wa Mbola kuufanya mradi huo kuwa endelevu kwa kutunza vizuri miradi yote
iliyoibuliwa kwa ajili ya uboreshaji wa maisha ya wananchi wa eneo hilo
.
Waziri huyo alitoa kauli
hiyo jana wilayani Uyui mkoani Tabora mara baada ya kuzindua maabara iliyochini
ya mradi huo ambayo imegharimiu shilingi milioni 49 hadi
kukamilika.
Alisema kuwa ni vema
wananchi hao wakahakikisha miradi yote iliyotekelezwa chini ya mradi wa vijiji
vya milenia wa Mbola inatunza vizuri ili iwe darasa la kufundishi vijiji vingine
hapa nchini katika utekelezaji wa malengo 8 ya milenia.
Dkt. Mgimwa aliongeza kuwa
itasikitisha kuona kuwa mara baada ya muda wa mradi kuisha wa 2006-2012 na
wafadhili ambao ni Milenia Promise Tanzania kumaliza muada wao na miradi inakufa
na kusema kuwa hatua hiyo haitakuwa nzuri.
Aidha alitoa wito kwa
wanavijiji wengine ambao hawapo katika mradi huo kwenda katika Kijiji cha
Ilolanguru wilayani Uyui ili wajifunze jinsi ya utekelezaji wa malengo ya
Milenia kwa kutumia juhudi za wananchi.
Awali akitoa taarifa kwa
Waziri wa fedha, Mwenyekiti wa Kijiji cha Ilolangulu Ally Magoha alisema kuwa
katika utekelezaji malengo ya Milenia chini ya mradi wa vijiji vya Milenia wa
Mbola wameweza kuboresha maisha yao katika vijiji 16 katika eneo
hilo.
Alitaja manufaa
waliyokwishapata ni pamoja na ujenzi wa nyumba za kisasa kwa kutumia matofali ya
kuchoma na bati na kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na
fedha.
Mogoha aliongeza kuwa pia
mradi huo umewawezesha kupunguza tatizo la vifo vya watoto waliopo chini ya
maika 5 na mamawajawazito ambapo awali vifo vilikuwa wastani wa watoto watatu(3)
hadi watano (5) na wanawake wajawazito 3 hadi 5 katika kipindi cha miezi mitatu
lakini hivi sasa vifo ni wastani huo katika kipindi cha miezi sita na wakati
mwingine hakuna.
Alisema kuwa hatua hii
imefikiwa mara baada ya kuwaelimisha wananchi juu ya kutumia vyandarua na kuua
mazalia ya mbu na hivyo kupunguza malaria katika eneo
hilo.
vilevile Mwenyekiti huyo
aliongeza kuwa kiwango cha wanafunzi wanaoishia njia(drop out) kimepungua mara
baada ya mradi huu kuanza kwani mbinu mbalimbali zimesaidia watoto wengi
kumaliza darasa la saba .
Mbinu hizo ni pamoja na
kutoa chakula kwa wanafunzi na kuhamasisha michezo mashuleni jambo liliwavutia
watoto wengi.
kuhusu suala la maji
alisema wanaendelea vizuri ambapo wastani wa asilimia 60 ya wakazi wa eneo hilo
wanapata maji safi na salama.
Mradi wa vijiji vya Milenia
wa Mbola unatelelezwa katika vijiji vya Ilolanguru, Isenga, Ngokolo, Ulimakafu,
Mpenge, Isila, Mbola, Kasisi A, Mabama, Ideka, Mbiti, Msiliembe, Iberi,
Inonalwa, Usagari, Msima na Migungumalo.


Post a Comment