WACHEZA sinema wenye majina makubwa Bongo, Wema Isaac
Sepetu na Aunt Ezekiel ‘Gwantwa’ wameingia kwenye bifu zito na kuwafanya
wasisalimiane.....
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu,
bifu la wawili hao lilianza usiku wa kuamkia Januari Mosi, mwaka huu baada ya
Wema kumwalika Aunt kwenye sherehe ya kuukaribisha mwaka lakini pamoja na
kuupokea mwaliko huo, Aunt hakutokea nyumbani kwa Wema ilikofanyika shughuli
hiyo iliyopambwa na vyakula na vinywaji.
Awali, Wema alipoona Aunt
anachelewa kufika kwenye shughuli hiyo, aliamua kumpigia simu mara kwa mara na
kupewa matumaini ya kuvuta subira.
Ilipotimu saa 6:01 usiku
bila ya Aunt kuonekana, Wema alimtumia ujumbe mzito kupitia mtandao wa BBM na
Aunt akaanza kuomba radhi.
Ujumbe wa Wema ulisomeka
hivi: “Hata sina hamu na wewe ila Happy New Year, sihitaji samahani yako sijui
niku-delete?”akimaanisha amuondoe kwenye orodha ya marafiki zake wa
karibu.
Mbali na ujumbe
huo, Risasi lina meseji za Aunt akimuomba radhi Wema kutokana na kutofika kwenye
sherehe hiyo.
Inadaiwa kuwa Wema
alikasirika na kuhisi kwamba Aunt aliungana na baadhi ya wasanii wengine wa
Bongo Movie ambao hakuwaalika kwenye shughuli yake kutokana na kupishana nao
Kiswahili siku za nyuma.
Asubuhi yake, Aunt aliandika
kwenye mtandao wa BBM: “ Chondechonde my luv, nimekosea mamy naomba unisamehe,
naomba msamaha mbele ya hadhara.”
Pamoja na kuombwa radhi,
Wema hakujibu kitu zaidi ya kumpotezea rafiki yake huyo aliyemsaidia kufanikisha
sherehe ya harusi yake iliyofanyika miezi michache
iliyopita.
Juzikati, mastaa hao
walikutana kwenye arobaini ya mama wa Mtangazaji wa Redio na Runinga za Clouds,
Zamaradi Mketema na wakashindwa hata kupeana salamu, kila mmoja alimchunia
mwenzake.
Mama mzazi wa Wema
aliendelea kumpiga stop mwanaye kwa kuwakumbatia marafiki, akamwambia kuwa hana
marafiki wa kweli.
Wema alipotafutwa ,
alishindwa kuweka wazi moja kwa moja kuwa haelewani na Aunt na kudai kuwa hana
muda wa kuongelea mambo hayo.
Kwa upande wake, Aunt
alikataa kutoa ushirikiano na kukata simu mara baada ya kuulizwa swali kuhusiana
na urafiki wake na Wema.
on Thursday, January 17, 2013
Post a Comment