Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Wenye nyumba za kupangisha kaeni tayari kulipa kodi!


 UONGOZI wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wamesema wanakuna vichwa juu ya  jinsi ambavyo watafanikisha kukusanya kodi kutoka kwa wenye nyumba nchini wanaofanya biashara ya kuzipangisha.

Kamishna Mkuu wa TRA, Harry Kitillya alisema jijini hapa mwishoni mwa wiki kwamba kuna changamoto nyingi katika ukusanyaji wa kodi kutoka kwenye nyumba zilizopangishwa.

Alisema ni kawaida kwa kila mtu anayepata fedha kihalali lazima alipe kodi, lakini utaratibu wa kudai kodi kutoka kwenye nyumba zilizopangishwa bado unatafutwa.

“Katika ukusanyaji wa kodi changamoto ipo kwenye kukusanya kodi inayotokana na biashara ya upangisaji, kwa sababu wenye nyumba wengine hawataki kuonyesha mikataba halisi, lakini sasa tumepata wazo tofauti ambalo tunalifanyia kazi ni kutafiti kwamba bei za nyumba za kupanga kulingana na eneo husika, mfano tukijua Masaki wanapangisha nyumba kwa kiasi gani tutakuwa tumepata pa kuanzia, pia tunataka kulifanya suala hili kwa kuhakikisha sheria inatumika ipasavyo,” alisema Kitillya.

Kitillya aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kumalizika kwa sherehe za Mahafali ya Tano ya Chuo cha Kodi, kilichopo jijini Dar es Salaam, ambapo wahitimu walikuwa ni 435 miongoni wakiwamo wanawake 137 sawa na asilimia 31.

Awali katika mahafali hayo Mwenyekiti wa Baraza la chuo hicho, Profesa Palamagamba Kabudi akitoa hotuba yake alisema katika kuhakikisha wanatoa huduma kwa wadau wote wa mfumo wa kodi udahili wa wanafunzi  umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka.

Alisema  hadi sasa chuo kimeweza kutoa jumla ya wahitimu 1,780 tangu mwaka 2007 kiliposajiliwa. “Chuo kimeweza kuingiza mapato ya Sh 3,333,043,499.44 kwa kipindi cha miaka minne, chuo kimejiwekea mpango wake ambao unaanza kutekelezwa katika mwaka ujao wa fedha’’ alisema.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Fedha, Saada Mkuya aliyekuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo,  katika hotuba yake aliwapongeza wahitimu hao na kuwataka watumie vyema ujuzi na maarifa  waliyopata kwa faida ya taifa, ikiwa ni pamoja na kuongeza ufanisi katika usimamizi wa kodi na kuwasaidia walipakodi watimize wajibu wao wa kulipa kodi kwa hiari.

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top