KITUO cha Mabasi yaendayo
mikoani na nchi jirani (UBT), kinakabiliwa na vitendo vya uhalifu, kutokana na
sehemu kubwa kukosa umeme iliyosababishwa na bomoabomoa ya kukihamishia Mbezi
Luis.Wakizungumza na Fullshangwe abiria na waangalizi wa mbasi kituoni
hapo, walisema unapofika usiku hali inakuwa ya kutisha kutokana na giza totoro
ambalo linawashawishi vibaka kuvamia eneo hilo.
Walisema miongoni mwa uhalifu unaofanywa
na vibaka hao, ni kuibiwa mafuta kwenye mbasi, vyuma vya majengo yaliovunjwa na
kuporwa abiria wanaofika usiku.
Alisema kabla kituo hakijavunjwa kila
mfanyabiashara alikuwa na mlinzi wake, hivi sasa eneo hilo liko wazi kitendo
kinachosababisha wezi kuongezeka.
“Usiku mnatisha unajua magari yenyewe
yanatisha yanapokuwa mengi, hakuna mwanga kitendo kinchochochea wezi kupata
maeneo ya kujifisha na kufanya vitendo vya uhalifu”alisema mmoja wa waangalizi
wa magari hayo.
Naye James John, alisema kwa sasa kituo
chote hakina umeme ukiondoa, jingo la polisi hali ambayo inasababisha huduma
zote usiku kuwa duni hata ile sehemu ya kupunzikia wasafiri na vyoo ambavyo ni
muhimu kwa wasafiri, ambako nako kuna giza.
“Tabu inakuwa alfajiri pale wasafiri
wanapofika kituoni hapo, kwani inatuwia vigumu kubaini haraka magari
tunayosafiri nayo kutokana na giza”alisema John.
Alipotafutwa Mkurugenzi wa Jiji Mussa
Zungiza ili kutoa ufafanuzi, ilielezwa kuwa yuko safarini nje ya nchi.
Post a Comment