Baadhi ya wachezaji wa timu ya
Yonga, wakiwa kwenye Uwanja wa Ndege wa jijini Mwanza leo asubuhi mara
baada ya kuwasili jijini humo kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa
kimataifa wa kirafiki na Black Leopards hapo kesho. Picha na Mtandao wa
Young Africans.
************************************
Timu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, leo asubuhi imewasili jijini
Mwanza kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wake wa kimataifa wa kirafiki
wa marudiano na timu ya Black Leopards, ya nchini Afrika ya Kusini,
mchezo unaotarajia kupigwa kesho kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini
humo.
Timu hiyo ya Yanga, ikiwa na msafara wa watu 37, wachezaji 27 na
viongozi 10 iliwasili majira ya saa 2 asubuhi Ndege ya Shirika la ndge
la Fast Jet ambapo leo jioni timu hiyo inatarajia kufanya mazoezi mepesi
katika Uwanja wa CCM Kirumba kwa ajili ya mchezo wa kesho.
Mchezo huo utakuwa ni wapili na wa mwisho wa kujipima nguvu kwa timu
hiyo ya Yanga, kabla ya kuanza mchakamchaka wa mzunguko wa pili wa Ligi
Kuu ya Tanzania Bara, unaotarajia kuanza Jumamosi ya Januari 26, mwaka
huu.
Katika mchezo wa kwanza baina ya timu hizo uliochezwa kwenye Uwanja
wa Taifa jijini Dar es Salaam, Yanga iliibuka kidedea kwa ushindi wa
mabao 3-2, huku mawili kati ya hayo yakiwekwa kimiani na Jerry Tegete,
na moja likifungwa na Frank Domayo.
Black Leopard amabyo inajiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu ya
PSL nchini Afrika Kusini iliomba kupata mchezo mwingine wa kirafiki
ambapo kampuni ya Prime Time Promotions walioandaa ziara ya timu hiyo
walikubaliana na Yanga mchezo huu ufanyike jijini Mwanza ili kutoa fursa
kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa kuweza kupata burudani ya soka kutoka kwa
timu hizi mbili.
Viiongillio vya mchezo huo vitakuwa ni Sh. 10,000/= kwa Jukwaa Kuu na Sh. 3,500/= kwa mzunguko.
on Tuesday, January 22, 2013
Post a Comment