Mahakama kuu kanda ya Mbeya
imemhukumu PETER MWAFRIKA mkazi wa Ndolezi wilayani Mbozi kunyongwa hadi kufa
baada ya kupatikana na hatia ya kuua kwa kukusudia.
Akisoma hukumu hiyo
iliyochukua saa 1.30 Jaji mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya mbeya NOEL CHOCHA
amesema licha ya mikono ya mahakama kufungwa kutoa adhabu ndogo kwa kosa la
maauaji ya kukusudia, pia adhabu hiyo ni hatua ya kukomesha watu wenye tabia
kama za mtuhumiwa kujichukulia hatua mikononi mwao.
Akirejea mazingira ya kesi
hiyo jaji Chocha amesema mnamo Februaly 11,2010 mshatakiwa na wenzake watatu
walifanya kosa la mauaji ya kukudia chini ya kifungu 196 chasheria ya mwenendo
wa makosa ya jinai kwa kumuua KOSAM MWAFRIKA ambaye ni kaka wa marehemu katika
kijiji cha Shaji kwa kumkata koromeo na kulitenganisha vipande
viwili.
Jaji Chocha katika maelezo
yake alisema mshtakiwa akiwa na wenzake ambao walitoweka baada ya mauaji hayo
walimvamia Kosam akiwa na mkewe shambani kwake eneo la Zanzule, Ndolezi na kisha
kumkamata marehemu kwa maelezo kuwa walikuwa wametumwa kumkamata ili wampeleke
polisi kwa kosa la wizi wa Ng'ombe.
Hata hivyo katika mabishano
shambani hapo, marehemu na wenzake walitamka wazi kuwa walikuwa wametumwa kumuua
marehemu hivyo kuongeza nguvu za ushahidi wa kumtia hatiani.
sababu za mauaji hayo ni
ugomvi wa muda mrefu uliokuwepo kati ya marehemu na mama yake mzazi wa mshtakiwa
ambao walikuwa wakigombea ardhi,(wote ni ndugu) na kwamba siku moja kabla ya
tukio hilo kulikuwa na kesi katika mahakama ya mwanzo Mlowo iliyokuwa
imefunguliwa na Mama mzazi wa mshatakiwa.
Inaelezwa pia kuwa wakiwa
njiani kumpeleka polisi, baada ya kubaini kuwa kuna watu wanawafuatilia ghafla
mtuhumiwa mwingine (ambaye hakuwepo mahakamani) alimkata marehemu panga la
shingo na kumfanya marehemu akose nguvu na kuanguka, hata hivyo kwa kuonyesha
kutoridhika na hali hiyo mtuhumiwa aliongezea kwa kumkata marehemu na panga
kwenye koromeo na kulitenganisha kabisa.
Jaji kabla ya kutoa hukumu
alirejea mazingira ya tukio hilo na kujiridhisha na miongozo, viini vya shauri
la mauaji na hoja zilizotolewa na washauri wa mahakama ambapo ilithitika kuwa
kulikuwa na dhamira ya mauaji na tendo la mauaji lilifanyika
Katika ushahidi wa shauri
hilo jumla ya mashahidi watatu waliletwa mahakamani akiwemo kaka wa mshtakiwa
ambao wawili kati yao walithibitisha pasipo shaka kwamba mshtakiwa Peter
kuhusika na tukio la kumuua kwakukusudia Kosam .
Katika utetezi wake wakili
wa mshtakiwa ZAKIA SULEIMAN aliiomba mahakama impe adhabu nafuu mshtakiwa
kutokana na umri wake mdogo hivyo mchango wake kuhitajika katika ujenzi wa
taifa, pamoja na kuwa na wategemezi wakiwemo wake wawili na watoto
wane.
Serikali iliwakilishwa na
Wakili Rogers Francis
katika hatua nyingine jaji
Chocha aliamua kufanya kazi ya kutoa elimu mahakamani humo, akirejea matukio
yaliyojitokeza hivi karibuni wilayani Momba na Mbozi aliyoyaita ni yanafanywa na
watu wasiopenda ama hawana habari na Utawala wa sheria yakiwemo kuwazika watu
wakiwa hai, ambapo amesisitiza hali hii inaonyesha kuwepo kwa watu waliovuka
kiwango cha ukatiri katika jamii.
amesema hali ya kushamiri mauaji wilaya za Mbozi na
Momba kuhaonyesha namna jamii na watu wenye tabia kama za mshitakiwa
wasivyopaswa kuvumilika mbele ya sheria na kwamba adhabu hiyo itasaidia
kuwaelimisha wengine wenye mitazamo kama ya mshtakiwa Peter
Mwafrika.
Habari kwa hisani ya Danny Tweve
Mbozi
|
Post a Comment