Kiungo wa
timu ya Azam FC, Bolou Kipre (kushoto) akitafuta mbinu za kumtoka
mshambuliaji wa El-Nasir FC ya Sudan ya Kusini, Abdallmelik Sebit,
wakati wa mchezo wa Kombe la Shirikisho uliochezwa leo kwenye Uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Azam, imeibuka na ushindi
wa mabao 3-1. Mabao ya Azam yamefungwa na Abdi Kassim, katika kipindi
cha kwanza, na mabao 2 yamefungwa na Kipre Tchetche katika kipindi cha
pili.
Wachezaji
wa Azam FC wakishangilia bao la pili la timu yao lililofungwa na Kipre
Tchetche (katikati) wakati ilipoibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya
El -Nasir ya Sudan ya Kusini katika mchezo wa Kombe la Shirikisho
uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kipre Tchetche (kushoto) akichuana kuwania mpira na beki wa Al-Nasri. |
Jabir
Aziz akitafuta mbinu za kuwatoka mabeki wa El Nasir FC ya Sudan ya
Kusini katika mchezo wa Kombe la Shirikisho uliofanyika leo kwenye
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mshambuliaji wa Azam FC, Brian Umomy akiwatoka walinzi wa timu ya El-Nasir FC ya Sudan ya Kusini, Jacob Osuru na Abdallmelik Sebit katika mchezo wa kombe la Shirikisho uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kikosi cha el Nasir ya Sudan ya Kusini
Kikosi cha Azam FC
Mashabiki wa Azam, wakishangilia
Post a Comment