|
Inspekta Jenerali wa Jeshi
la Polisi Nchini (IGP) Said Mwema (kulia) Waziri wa Mambo ya ndani Emmanuel
Nchimbi na Kamnda wa Pilisi Zanzibar Ally Mussa kwenye moja ya mikutano na
waandishi wa habari.
*********** SIKU chache baada ya kutokea kifo cha Padri
Evarist Gabriel Mushi kupigwa risasi na watu wasiojulikana kichwani eneo la Beit
el Raas, Jana Imamu wa Msikiti wa Mwakaje ameuawa baada ya kupigwa mapanga hadi
kufa. Kwa
mujibu wa maelezo ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja, Ahmada Khamis
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo hapo jana mchana majira ya saa 8 na kumtaja
aliyefariki kuwa ni Sheikh Ali Khamis ambaye ameuawa na watu
wasiojulikana. Kamanda Ahmada alisema
Sheikh Khamis mbali ya kuwa ni Imamu wa Msikiti lakini pia ni mkulima na
ameuliwa wakati akiwa katika mazingira ya kazi zake ndani ya shamba lake huko
Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja. Akielezea mazingira ya tukio hilo Kamanda Ahmada
alisema tukio hilo limetokea baada ya Sheikh Khamis kwenda shambani kwake katika
shmba la minazi Kidoti ambapo wakati akiwa shambani hapo ndipo walipotokea watu
kadhaa na kumpiga mapanga sehemu za shingoni mwake na kusababisha kifo chake
muda mfupi baada ya kipigo hicho. Alisema baada ya tukio hilo, watu walimchukua na
kumkimbiza hospitali lakini kutokana na kupoteza damu nyingi alifariki dunia
wakati akiwa njiani na hivyo harakati za mazishi zinafanyika baada ya
kuchukuliwa vipimo na wataalamu wa afya. Kamanda Ahmada ametoa wito kwa wananchi kutopuuzia
taarifa za watu ambao wanawashuku na wenye kuleta maafa yakiwemo mauaji hapa
nchini, kwani kuwaficha wahalifu ni kuendeleza utamaduni usiofaa katika jamii
ambayo imeanza kuharibika kutokana na mauaji hayo yanayoendelea kila
kukicha. Hili ni tukio la nne kwa
viongozi wa dini kuhujumiwa ambapo tukio la kwanza Sheikh Fadhil Suleiman Soraga
kumwagiwa tindi kali na watu wasiojulikana na kujeruhiwa vibaya wakati akifanya
mazoezi nyakati za asubuhi karibu na nyumbani kwake Magomeni, tukio la pili ni
lile la Padri Ambrose Mkenda aliyepigwa mapanga shingoni na kurejuhiwa vibaya na
watu wasiojulikana wakati akitaka kuingia nyumbani kwake huko Tomondo Mjini
Unguja. matukio hayo mawili yalitokea mwaka jana. Katika mwaka huu nako kumetokea matukio mawili kwa
kuuawa kwa Pardi Evarist Mushi huko Beit El Raas wakati akitaka kuingia Kanisani
na pia kuuawa kwa Sheikh Ali Khamis huko Kidoti shambani kwake Mkoa wa
Kaskanizini Unguja. Inna lillahi wainna ilayhi rajiiun. |
on Sunday, February 24, 2013
Post a Comment