Jengo kuu la Ghorofa 5
ambalo lilikuwa halijamalizika ujenzi wake lililopo eneo la Sinza Mori karibu
kabisa na Masjid Qubah,limeporomoka jioni hii na kusababisha kifo cha mtu mmoja
ambaye alikuwa na wenzake wawili jirani na jengo hilo,ambapo mmoja alivyoona
hatari hiyo alikimbia na kuwaacha wenzie wawili ambao walinasa ndani.
Kati ya walionasa mmoja
amefanikiwa kutolewa huku akiwa ameumia vibaya na mwingine ndio huyo aliepoteza
maisha.
Inasemekana chanzo cha
kuanguka kwa jengo hilo la Ghorofa ni hali yake ya kukaa kwa muda mrefu bila
kumalizika kwa ujenzi waka ambapo inadaiwa kuwa lina umri wa zaidi ya miaka 10.
Habari kamili na picha za tukio lenyewe zitafuata
baadae kidogo.
......... Endelea kuwa na NDGSHILATU BLOG mahala popote na wakati wowote .......
Post a Comment