Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

BREAKING NEWZZZ!!! JENGO LA PPF TOWER LINAWAKA MOTO HUU

 





Taarifa zilizotufikia hivi punde ni kwamba jengo la PPF TOWER maeneo ya Posta Mpya ,barabara ya OHIO lina waka moto.

Moto umeanza kuwaka ghorofa ya juu kabisa ndiko moshi uonaonekana ukitokea.Kikosi cha FIRE kimesha fika kijaribu kuuzima moto huo.

chanzo cha moto hadi sasa hakijafahamika nini?.

Tukio hilo limetokea majira ya saa 1.30 asubuhi ya leo baada ya walinzi wa jengo hilo kushuhudia moshi mzito ukitoka kutoka ndani ya jengo hilo katika ghorofa ya mwisho na hivyo kulazimika kutoa taarifa vikosi vya zimamoto .

Hata hivyo inadaiwa kuwa kikosi cha jeshi la zimamoto na uokoaji wamefika mapema zaidi eneo la tukio na askari wake kufanikiwa kupanda hadi juu ya ghorofa hiyo ambako moto huo ulianzia kuwaka ili kujaribu kuzima japo shida kubwa ni mpira wa maji kufika katika eneo hilo.

Kwani katika eneo hilo ambako pia kuna mitambo mbali mbali ya mawasiliano imefungwa ila mbali ya kutumia winchi kupandisha mpira huo wa maji bado imekuwa ngumu kufika juu ya ghorofa hilo.

Hivyo moja kati ya changamoto ambazo zimetajwa kwa wajenzi wa majengo ya ghorofa jijini hapo ni kujenga majengo hayo huku wakichukua tahadhari na matukio ya moto pia .

Hadi sasa eneo la tukio askari wametanda kila kona ili kupambana na vibaka ambao wamekuwa na kawaida ya kupora mali katika maeneo ya matukio kama hayo na kuwa hakuna madhara yaliyojitokeza kwa binadamu japo thamani ya mali zinazoendelea kuteketea bado kujulikana na jitihada za kuzima moto zinaendelea

Kusema kweli mazingira ni magumu sana ya uzimaji wa moto huo kutokana na urefu wa jengi lenyewe.

Taarifa zaidi kukujia hivi punde ..... Endelea kuwa na NDGSHILATU BLOG mahala popote na wakati wowote .....
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top