|
Mkuu wa
wilaya ya Ilemela Bi. Amina Masenza akishuhudia mlundikano wa magodoro na hali
ya sehemu wanayolala wavulana wa shule ya Mount Zion kwenye moja ya vyumba vya
darasa vilivyotengwa kwa ajili ya
kujisitiri. |
ZIARA ya kushitukiza
iliyofanywa na Mkuu wa wilaya ya Ilemela Bi. Amina Masenza akiambatana na
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama kufanya ukaguzi katika shule ya sekondari
ya Mount Zion iliyoko ilemela jijini Mwanza imebaini wanafunzi kuishi katika
mazingira hatarishi huku uongozi wa shule hiyo ukiwaficha vichakani zaidi ya
wanafunzi 50 wa bweni kukwepa ukaguzi.
Hatua hiyo inafuatia
kuwepo taarifa zilizotolewa kwa mkuu huyo na baadhi ya wasamaria wema hali
iliyomlazimu mkuu wa wilaya na ujumbe wake kufika shuleni hapo ili kujionea
endapo uongozi wa shule hiyo umeboresha kasoro na mapungufu yaliyoonekana baada
ya ukaguzi wa awali kufanyika kwa kipindi cha mwezi mmoja uliopita baada ya
kutakiwa kuyafanyia kazi mapungufu hayo na Idara ya Afya na Elimu
ukaguzi.
|
Mkuu wa
wilaya ya Ilemela Bi. Amina Masenza alishuhudia jinsi hali mbaya kwa vyoo
vilivyounganishwa ndani ya bweni njia zikiwa zimebananishwa na masanduku ya bati
ya kuhifadhia nguo za wanafunzi bila kuwa na usalama wa
kiafya. |
|
Wanafunzi
50 waliobainika kufichwa waumbuliwa. |
Hata hivyo jeshi la
polisi baada ya kupata taarifa hizo nalo lilifuatilia na kufanya msako kwenye
vichaka vinavyozunguka shule hiyo na kufanikiwa kuwakuta wanafunzi hao wakiwa
wamejificha chini ya ulinzi wa mmoja kati ya waalimu wa shule hiyo kisha
kuwaamuru kwenda shuleni ambapo mkuu wa wilaya na ujumbe wake walikuwa
wakizungumza na uongozi wa shule na wanafunzi wengine hali iliyo
washangaza.
|
Msafara
wa wanafunzi wa kidato cha kwanza waliojificha na mwalimu wao kukwepa kukutwa
wakiwa wamekalia ndoo kwenye msongamano madarasani ukirejeshwa shuleni chini ya
uangalizi wa maafisa wa jeshi la polisi nyuma na mbele ya
msafara. |
Akizungumza huku machozi
yakimbubujika kwa uchungu wa hali aliyoishuhudia shuleni hapo Mkuu wa wilaya ya
Ilemela Bi. Amina Masenza ameeleza kusikitishwa kwa kitendo hicho na kukilaani
vikali akiagiza hatua madhubuti za kisheria kuchukuliwa dhidi ya Mkurugenzi wa
shule hiyo….
|
Hii ndiyo
hali halisi ya ukaaji ndani ya darasa hili jeh kwa mpango huu kuna usalama wa
kufanya vyema kazi za darasani na hatimaye kufaulu kwenye mitiani
kihalali? |
|
Shule ya
Sekondari ya Mount Zion ina jumla ya vyumba 7 vya madarasa ambavyo ilisajiliwa
navyo kuhudumia wanafunzi 160, madarasa yakibaki idadi hiyo, wanafunzi
wameongezeka na kuwa 515 hali inayosababisha msongamano mkubwa wa wanafunzi
darasani kiasi cha madarasa mengine kuwa na wanafunzi hadi 119 nao wanafunzi
wengine wakilazimika kutumia ndoo kama viti kutokana na uhaba wa mkubwa wa
madawati. |
|
Fanya
tahtimini ya haraka kwa kila hali ya mwanafunzi huyu wa shule ya Mount Zion
anayetumia mapaja yake kama dawati, ndoo kama kiti cha kukalia, chini akiwa na
malapa... Ingawa anatabasamu sijui kichwani anawaza nini.... je kwa staili hii
tunapaswa kushangaa juu ya matokeo ya kushuka kiwango cha elimu yanayozuka kila
miaka? |
|
'Back
bencha' |
|
Wanafunzi
wanao soma shuleni hapa wengi wanatoka mikoa mbalimbali hapa nchini, hilo
lilibainika kupitia mjumbe huyu aliyekuwa akiwauliza wanafunzi hao. Mikoa
waliyotaja kutoka ni pamoja na Shinyanga, Mara, Kagera, Dodoma, Mbeya, Morogoro,
Tanga na hata Dar es salaam wapo, kiasi kwamba akawauliza je mlishakalia ndoo au
viti vya plastiki hata kwenye shule za msingi mlizotokea? jibu likawa
HAPANA |
|
Hifadhi
ya masanduku ya wanafunzi wengine waliosongamana kwenye hosteli iliyo mbali
kidogo na shuleni hapo. |
|
Nje ya
hosteli. |
|
Ni
mlundikano wa magodoro chini na hali halisi ya mazingira ya sehemu wanayolala
wavulana wa shule ya Mount Zion kwenye moja ya vyumba vya darasa vilivyotengwa
kwaajili ya kujisitiri hali inayoshtusha juu ya uwekaji wa neti kujikinga na
malaria. |
|
Ni ndani
ya moja ya chumba kidogo cha wasichana ambacho ndani yake kuna matandiko haya
sambamba na masanduku 13 ikimaanisha ndiyo idadi ya wasichana wanao lala
chumbani hiki. |
|
Ndani ya
chumba kingine kidogo kwa bweni la wasichana na hii ni style ya kuhifadhi
magodoro ya walalaji humu. |
|
Kamati ya
ulinzi na usalama ya wilaya ya ilemela ikikagua shimo la maji taka ambapo
ilibaini bomba kutoka kwenye septik tank kuungwa kwa umbali mrefu hadi sehemu ya
wazi na kuyaruhusu maji taka na kinyesi kibichi kumwagika hovyo juu ya ardhi
kiasi cha kuweka hali hatarishi kwa afya na urahisi wa mlipuko wa magonjwa kwa
wanafuzni na wananchi majirani wa eneo la
shule. |
|
Akiwa
amepakizwa kwenye pikipiki kuelekea zahanati ya jeshi iliyo karibu na eneo la
shule, mwanafunzi huyu aliyejitambulisha kwa taabu kwa jina la Takiu Kitundu,
aliyekuwa hoi akiumwa alikutana njiani na msafara wa kamati ya ulinzi na usalama
ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya Bi Amina Masenza, ndipo mkuu huyo akaamuru moja
kati ya magari kwenye msafara wake kumuwahisha mwanafunzi huyo
hospitali. |
|
Mwanafunzi
mgonjwa akipakiwa kwenye gari la msafara kuwahishwa
hospitali. |
|
Dr.
Daniel Batane akisoma agizo la ofisi ya Afya wilaya kuifunga mara moja shule
hiyo. |
Akisoma Ilani ya
Kisheria ya kusitisha shughuli za utoaji elimu kwa shule hiyo mbele ya Mkuu wa
wilaya hiyo na Afisa Elimu Sekondari wa Manispaa ya Ilemela, Afisa Afya wa
Manispaa ya Wilaya ya Ilemela Dr.Daniel Batane amesema kuwa kupitia ukaguzi wa
kiafya uliofanyika tarehe 13/02/2013 na kufanywa na maofisa Afya kutoka manispaa
na kata husika madhaifu mengi yalibainika.
Moja kati ya kasoro
zilizoainishwa ni pamoja na mfumo wa maji taka na vyoo ulikutwa ukiwa umejaa
hadi kutapisha na pia ni mdogo sana kiasi cha kushindwa kukidhi mahitaji ya
idadi ya wanafunzi wote 515 wa jinsia zote.
Pia shule hiyo
imegundulika kutokuwa na shimo la maji taka kiasi chakuelekeza bomba kutoka
kwenye septic tank kwenda kwenye eneo la wazi huku ukimwaga kinyesi kibichi na
kusababisha kero kubwa ya harufu kali pamoja na kuweka mazingira hatarishi ya
uwezekano wa kuzuka kwa magonjwa ya mlipuko.
Mazingira ya kuhudumia
chakula katika shule hiyo yalikutwa hatarishi kiafya, panya wengi wakizagaa
kwenye stoo ya chakula sambamba na ushahidi wa panya kukutwa akiwa amefia ndani
ya diaba lililokuwa linatumika kuhifadhia maji ya
dharura.
Mapungufu mengine
yaliyobainishwa ni pamoja na shule hiyo kukosa mabweni rasmi kwa malazi ya
wanafunzi zaidi ya kuwa na darasa moja linalotumika kama sehemu ya kulala
wanafunzi wavulana.
-Kukosekana kwa vitanda
katika vyumba vya wasichana kiasi cha kuwafanya kulala chini kwenye magodoro
yaliyochakaa huku hali ya usafi katika vyumba hivyo ikiwa mbaya kutokana na
msongamano usiotoa nafasi kwa usafi kufanyika ipasavyo.
Kufuatia sakata hilo
Idara ya Afya Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela jijini Mwanza imetoa agizo la
kisheria kuifungia mara moja shule ya Sekondari ya Mount Zion kutokana na
kukiuka kanuni za uendeshaji wa shule pamoja na shule hiyo kukithiri kwa uchafu
suala ambalo ni kinyume cha sheria ya Afya ya jamii no. 1 ya mwaka
2009.
Post a Comment