Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

DC MUSHI AELEZEA MAFANIKIO YA WILAYA YA ILALA

DSC02989Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw, Raymond Mushi,akielezea mafanikio ya Serikali ya awamu ya nne kwa kipindi hicho katika wilaya hiyo.

 

Mushi amesema kuwa, Kiwango cha uzoaji taka ngumu kimefikia tani 550 kwa siku sawa na tani 198,000 kwa Mwaka ambapo amesema kiwango hicho ni asilimia 50% ya tani 1100 za taka zinazo zalishwa kwa siku.
“Kwa sasa kiwango cha Uzoaji taka ngumu kinaridhisha kutokana na wilaya kupata vitendea kazi vyenye uwezo Mzuri”, amesema Mkuu wa Wilaya.
Amesema kuwa Mafanikio hayo, ni Miongoni mwa Mafanikio Mengi ambayo Serikali hiyo imeyafikia kwa kipindi chake tangu imeingia Madarakani na kusema kuwa wana matumaini kuwa mpaka kufikia mwaka 2015, Manispaa hiyo itakuwa imefanikisha Mengi.
Ameendelea kusema kuwa, kufanikiwa kwa asilimia hizo kunachangiwa na kununuliwa kwa Magari sita ya kukandamiza taka yenye Uwezo Mkubwa wa kubeba kati ya tani kumi hadi 24 kwa Safari moja ikiwa ni pamoja na Kununuliwa kwa makasha ya taka 30 na kuwekwa kwenye maeneo yenye uzalishaji Mkubwa wa taka.

Ameendelea kuyataja Mafanikio mengine yaliyopo katika Manispaa hiyo kwa kipindi cha mwaka 2005-2012 kuwa ni, Usambazaji maji ambapo amesema katika Mamlaka ya maji DAWASA imeongeza visima virefu vya Maji kutoka visima 110 mwaka 2005 kufikia 195 na visima vifupi 60 kwa mwaka 2012.
Amesema kuwa, mafanikio hayo yameambatana na Uboreshwaji wa Huduma za Afya, Ardhi, Kilimo Ujenzi pamoja na Elimu, ambapo Katika Afya Manispaa imefanikiwa kuongeza idadi ya Vituo vya kutolea huduma kutoka 15 hadi 22 pamoja na Zahanati 20 kutoka 13 zilizokuwepo kwa mwaka 2005-2012
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top