Dereva
wa Lori la Maji wa Kampuni ya Dolfin yenye maskani yake Mbezi Tang Bovu, jijini
Dar es Salaam,ambaye hakuweza kufahamika jina lake mapema, akiugulia maumivu
baada ya kupigwa na kuumizwa na jamaa wawili waliokuwa na kina dada wawili
katika gari ndogo eneo la Mbezi njia inayoingia katika Shule ya Mbezi Beach
Sekondari jana usiku.
Dereva
huyu alikuwa akitokea Barabara kubwa akiingia katika njia ndogo inayoelekea
Shule ya Sekondari ya Mbezi Beach, na gari ndogo ilikuwa ikitokea katika njia
hiyo ndogo na kukutana uso kwa uso na lori hilo, huku watu waliokuwa katika gari
hiyo ndogo wakimtaka dereva wa lori kuwapisha wao ili waanze
kupita.
Dereva
huyu aliamua kubana kushoto na kuwaachia njia ili wapite, kama picha ya Lori
inavyoonyesha chini, laiki jamaa waliokuwa katika gari ndogo waliamua kushuka na
kumshusha dereva huyo na kisha kuanza kumshambulia kwa magumi na mawe, huku
dereva huyo akitoka nduki na kuacha gari lake, hadi katikati ya barabara
inayoelekea Tegeta ikitokea Mwenge, walipomtia mikonini na kuanza kumpiga kama
mwizi huku wakitumia mawe kumpigia kama makwenzi, na kumuumiza kama hivi, hadi
walipofika watu kibao na kuanza kuamulizia ugomvi huku wakijua kuwa jamaa huyo
ni mwizi huku wengine wakijandaa kunza kumshambulia.
Lakini
watu hao baada ya kupata stoti kamili ilivyokuwa waliamua kuwageuzia kibao watu
hao wakianza kuwasonga kutaka kuwashambulia ndipo walipoamua kudandia gari na
kukimbia, huku mmoja kati ya wanawake waliokuwa na jamaa hao, akisikika
kumwambia jamaa huyo,
''usirudie
kutukana watu waliovaa suti hovyo bila kuwajua watakuua''.
Gari
hiyo wakati ikianza kuondoka eneo hilo hukuikiendeshwa na mwanamama, ilianza
kushambuliwa kwa mawe kwa bahati iliwahi kuondoka eneo hilo na kuingia usawa wa
Barabara ya Masana na kutokomea.
Watu
hao wakidandia gari iliyoanza kutembea ili kutoweka eneo hilo.
Jamaa
hao wakianza kuondoka eneo hilo kwa kasi huku gari hiyo ikiendeshwa na
Mwanamama.
Lori
lililozua kasheshe hilo, ndiyo hili na eneo lenyewe ndo kama hivi linavyoonekana
huku magari yakiwa na uwezo wa kupita bila kugusana na lori
hilo.
Lori
hilo likiwa limeachwa katika eneo la tukio baada ya dereva wake kupewa kipondo
huku magari mengine yakipita kama kawaida.
Post a Comment