Waziri Mkuu Mstaafu Edward
Lowassa
---
WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa,
ametamba kuwa anajisikia furaha kwa kutimiza ndoto yake ya kuujengea uwezo,
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi, (UVCCM), ndiyo maana akaomba
asichaguliwe tena kwenye nafasi ya Mwenyekiti wa Baraza la Udhamini la umoja
huo.
Akizungumza ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana, Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, alisema amekuwa mwenyekiti wa baraza hilo kwa miaka 15 na kwamba ameliongoza kwa mafanikio.
“ Niliomba mwenyewe kuondoka, niliwaeleza kuwa nisingependa kuendelea tena kuongoza baraza hilo nina mambo mengine ya kufanya, nilikuwa na ndoto za kuwafikisha mahali ambapo wanaweza kujitegemea, mwisho wanihesabu kuwa mimi ni mtumishi nisiye na faida, nimefanya yale yaliyonipasa, nimefanikiwa,” alisema Lowassa.
“Mafanikio makubwa ni pamoja na kuwawezesha vijana kujitegemea, kwa kuweza kumiliki jengo la uwekezaji, kwa fedha wanazozipata huko wanaweza kujilipa mishahara yao wenyewe, ni mradi mkubwa ambao hata chama chenyewe hakina,” alisisitiza. Kwa Habari zaidi bofya na Endelea......>>>>>>
Post a Comment