Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Mwenyekiti wa Chama
cha Mapinduzi CCM Dk. Jakaya Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakisalimiana
na wafanyakazi wa ndege ya Rais mara baada ya kushuka kwenye ndege alipowasili
katika uwanja wa ndege wa Kigoma leo jioni, kwa ajili ya sherehe za miaka 36 ya
CCM zitakazofanyika kesho kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma na
kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho pamoja na viongozi wa vyama
rafiki vya CCM kutoka nchi jirani za Burundi na DRC Congo.
Rais Jakaya Kikwete akivishwa skafumara baada ya kuwasili kwenye
uwanja wa ndege wa Kigoma leo jioni kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM
Bara Mzee Philip Mangula na katikati ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman
Kinana.
Ndege iliyomleta Rais Jakaya Kikwete ikiwasili kwenye uwanja wa
ndege wa Kigoma leo jioni huku ikilakiwa na wananchi waliojitokeza kumpokea
Rais.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Shaaban Kirumbe Mjumbe wa
NEC Wilaya ya Kigoma mjini, kulia ni Peter Selukamba Mbunge wa Jimbo la Kigoma
mjini.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na wananchi mbalimbali
waliojitokeza kumlaki kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma.
Rais Jakaya Kikwete akiwa amembeba mtoto Khalfan Majjid
huku akizungumza naye kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma kushoto ni Baba mzazi wa
mtoto huyo Majjid Khalfan.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Nape Nnauye Katibu
wa Halmashauri Kuu ya CCM Itikadi na Uenezi mara baada ya kuwasili mjini Kigoma
leo.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na wananchi mbalimbali
waliojitokeza kumlaki kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na wananchi mbalimbali
waliojitokeza kumlaki kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, na
Rais Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mzee
Mwilima.
Wadau kutoka CCM Makao Mkuu kutoka kulia ni Lusekelo,Dr.
Alice,Hassan,Jestina na Beatus wakishoo Love wakati wa mapokezi ya Rais Jakaya
Kikwete katika uwanja wa ndege wa Kigoma.
Mwigulu Nchema Naibu katibu Mkuu Bara CCM akisalimiana na
Asha-Rose Migiro Katibu wa Halmashauri Kuu Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wakati
wa mapokezi ya Rais Jakaya Kikwete , Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Kibondo
Venance Mwamoto.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akijadiliana
Jambo na Daniel Sanzugwako mjumbe wa NEC CCM Kasulu.






















Post a Comment