KAULI JUU
YA MAUAJI YA PADRI EVARISTUS MUSHI
Vijana wenzangu na wasomaji wa makala.
Hivi karibuni kuna vitendo vimeanz kujijenga katika jamii yetu ambayo havitoi
ishara nzuri tuendako.
Matukio ya kupigwa risasi padri na kuchomwa
makanisa na harakati za muamsho. Haya yote pamoja na yaliyotokea geita si mambo
ya kufumbiwa macho. Ninaomba niwasihi watanzania wenzangu kuwa haya si mambo
yanayoweza kutuimarisha katika umoja na mshikamano wetu. Niwasihi tena kukumbuka
kuwa umoja na mshikamano wetu haukuja kama ajali ni misingi ambayo wazee na
waasisi wa nchi zetu walikubaliana na kuimarika katika mioyo yao, tusidharau na
wala tusibeze.
Mwisho nirudie kuwaomba nikiwakumbusha kauli ya Raisi wetu
wa jamhuri ya Muungano kuwa ".... Hivi ni vitendo ambavyo sisi wenyewe
tunavipanga. Ni jukumu letu viongozi wa dini,wanaharakati na wanasiasa kukemea
haya. Endapo tutaamua kukemea haya kwa vitendo havitaendelea."
Poleni
sana waumini wa dini kwa kupoteza kiongozi wenu nami naungana nami katika
kuomboleza na NINALAANI kitendo
hiki
on Monday, February 18, 2013
Post a Comment