Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akizungumza ofisini kwake na Msajili wa
Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR), Bongani Majola
(katikati). Ziara hiyo, ambayo pia ilikuwa na lengo la msajili huyo
kujitambulisha na kumsalimia Waziri Nchimbi, na kumuelezea shughuli mbalimbali
zifanywazo na mahakama hiyo pamoja na kumuelezea changamoto mbalimbali
zinazoikabili mahakama hiyo. Hata hivyo, Waziri Nchimbi aliahidi kushirikiana na
mahakama wakati wowote itakapohitaji msaada kutoka ofisini
kwake.
Msajili wa Mahakama ya
Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR), Bongani Majola (katikati)
akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto)
kuhusiana na mafanikio na changamoto mbalimbali ya Mahakama hiyo ambayo Makao
Makuu yake yapo jijini Arusha. Kulia ni Msemaji wa Mahakama hiyo, Roland
Amoussouga.
Msemaji
wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR), Roland
Amoussouga akimfafanulia masuala mbalimbali Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk
Emmanuel Nchimbi (kushoto) wakati viongozi hao walipomtembelea waziri huyo
ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo. Wa pili kutoka kushoto ni Msajili wa
Mahakama hiyo, Bongani Majola. Kulia ni Mwanasheria wa mahakama hiyo, Jerry
Mburi.
PICHA ZOTE
NA
KITENGO
CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
YA NCHI.
Post a Comment