Kundi la Nyumbu madume wakiwa wamejikusanya pamoja Serengeti wakiangalia watoto wao wanavyofurahia mandhari ya Serengeti
Ndama huyu wa nyumbu hachezi mbali na mama yake kwa ajili ya kunyonya.Picha Kwa Hisani Ya Fullshangwe Blog
………………………………………………………………
Zaidi ya Watalii 16,500 kutoka
mataifa mbalimbali ulimwenguni miongoni mwao wakiwemo Watanzania 5,800
wamefurika katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa ajili ya kushuhudia
tukio adimu linalohusisha Nyumbu wapatao elfu nane (8,000) kuzaliwa kila
siku.
Mwezi Februari kila mwaka ndipo
msafara wa Nyumbu hufika katika eneo la kusini mwa Serengeti kwa ajili
ya kuzaliana. Miongoni mwa wageni waliofika Serengeti mwaka huu
kushuhudia tukio hili muhimu ni pamoja na watafiti wa wanyamapori na
wanazoolojia wanasayansi maarufu sana ulimwenguni.
Msimu wa Kuzaliana katika
Serengeti ni tukio la kipekee ambapo ni Serengeti pekee duniani ambapo
wanyama hawa huzaliana kwa pamoja katika mzunguko wao wa mwaka mzima.
Msimu huu wa kuzaliana utadumu
kwa muda wiki sita ambapo hadi kukamilika kwake inatarajiwa kuwa ndama
wapatao 500,000 watakuwa wamezaliwa katika eneo la Serengeti ambayo ni
hifadhi ya pili kwa ukubwa nchini Tanzania.Kinchosisimua zaidi katika
tukio hili ni pale ambapo nyumbu hawahitaji kulala chini kwa ajili ya
kuzaa bali tukio hili huendelea huku Nyumbu akiwa anaendelea kutembea na
kula malisho ya majani hifadhini.
Cha kipekee zaidi ni pale ndama
aliyezaliwa mara tu akishazaliwa, humchukua kati ya dakika mbili hadi
tatu kuanza kurukaruka na kumfuata mama yake kwa kasi kubwa.
Hata hivyo miongoni mwa ndama
hawa wanaozaliwa kipindi hiki, wengi wao wapo hatarini kuliwa na wanyama
wakali wanaowawinda kwa hamu kubwa kwa ajili ya kujipatia chakula.
Wanyama hawa maarufu kwa kuwinda ndama hawa ni pamoja na fisi wanaofikia
7,500 pamoja na simba zaidi ya 3,000 ambao wote hukodolea macho tukio
hili kwa nia ya kujipatia mlo wao.
Post a Comment