Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MAHAKAMA YA WATOTO YAFUNGULIWA ZANZIBAR

 


indexNa  Khadija Khamis-Maelezo Zanzibar
…………………………………..
 JAJI Mkuu wa ZanzĂ­bar Omar Othmani Makungu amesema  kuwepo kwa Mahakama ya watoto nchini kutasaidia kupunguza mrundikano wa kesi zinazowakabili watoto mahakamani na kupatikana haki zao kwa wakati.
 Jaji Makungu ameyasema hayo alipokuwa akifungua Mahakama ya Watoto Zanzibar huko Vuga ikiwa ni shamra shamra ya siku ya Sheria duniani inayoazimishwa Februari 7 kila mwaka.
 Amesema lengo la kufunguliwa Mahakama hiyo ni kukabiliana na changamoto ya ongezeko la kesi zinazohusu Watoto na kuwapatia haki zao za msingi kwa wakati.
 Aidha ameongeza kuwa Mahakama hiyo itakuwa ni mazingira rafiki kwa watoto ambayo yatawasaidia kuweza kujieleza pamoja na kutoa ushahidi bila ya hofu.
 Jaji Makungu amefahamisha kuwa wanatarajia kuanzisha Mahakama ya Watoto kwa upande wa Pemba sambamba na kuweka mahakama ndogo ndogo katika kila wilaya ili kuweza kuondoa usumbufu kwa wananchi.
 Nae katibu Mkuu Wizara ya Ustawi wa Jamii maendeleo ya Wanawake na Watoto Fatma Gharib Bilali amewataka wazee kushirikiana na mahakama hiyo ili kuweza kutatua matatizo mbali mbali yanayowakabili watoto ikiwemo kurekebisha tabia na kukufatilia nyendo zao.
 “Maendeleo yeyote lazima yawe na changamoto zake jamii lazima iwasaidie watoto kuwalinda na vishawishi vya watu wabaya” alisema Katibu huyo.
 Nao Wawakilishi kutoka Mashirika ya Kimataifa ya UNICEF na Save The Children wameishukuru Mahakama Zanzibar kwa ushirikano wao wa kuweza kuanzisha mahakama ya watoto ambayo itaweza kutetea na kulinda haki za mtoto na ustawi wake.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top