Mkuu
wa Upelelezi Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Duwani Nyanda akizungumza na viongozi
wa Kanisa la Moravian Jimbo la Misheni
Mashariki |
Uamuzi huo ulitolewa jana na Jaji Mathew
Mwaimu,baada ya bodi hiyo ya wadhami wa Kanisa la Moravian Kusini chini ya
Mchungaji Clement Mwaitebele, kupitia wakili wao, Henry Chaula wa Kampuni ya
Uwakili ya C&M, kufungua kesi namba 12 ya mwaka 2013 na kuomba isikilizwe
chini ya hati ya dharura.
Kwa mujibu wa kesi hiyo, Mchungaji Gervas
Mwakafwila, Mchungaji Silas Mwakibinga, Tukuswiga Mwakabur, Atuganile Mbombo,
Isakwisa Ernest na Sekela Mukisele ambao wanatetewa na Wakili Benjamin
Mwakaganda wa Kampuni ya uwakili ya BM, wanadaiwa kufunga makufuli kwenye
Kanisa la Usharika wa Tabata, ili kuzuia bodi hiyo kumsimika mchungaji
mpya.
Akitoa uamuzi, Jaji Mwaimu alikataa ombi la bodi
hiyo ya wadhamini la kutaka kufunguliwa kwa makufuli yaliyokuwa yamefungwa
kwenye kanisa hilo, ili kupisha kumsimika mchungaji mpya.
Pia jaji huyo aliruhusu shughuli za kawaida za kanisani hapo kuendelea na kusisitiza kwamba kilichozuiwa ni usimikaji wa mchungaji ili kuondoa uvunjifu wa amani.
Pia jaji huyo aliruhusu shughuli za kawaida za kanisani hapo kuendelea na kusisitiza kwamba kilichozuiwa ni usimikaji wa mchungaji ili kuondoa uvunjifu wa amani.
Baada ya kutoa uamuzi huo, Jaji Mwaimu aliwataka
wadaiwa kupeleka kiapo pinzani mnamo au kabla ya Februari 5, mwaka huu ambapo
kesi hiyo imepangwa kusikilizwa.
Bodi hiyo ya wadhamini wa Kanisa la Moravian
Jimbo la Rungwe ni wadaiwa namba 4 katika kesi namba 222 iliyofunguliwa mwaka
2012 katika Mahakama Kuu, ambayo inaendelea kusikilizwa Februari 6, mwaka huu
mbele ya Jaji Augustini Mwarija.
Katika kesi hiyo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Jimbo la Mashariki na Pwani ya Kanisa la Moravian Tanzania, Clement Fumbo na
wenzake saba wanapinga kuondolewa madarakani na kusimamishwa
kazi.
Katika kesi hiyo, Fumbo na wenzake hao saba
wanaiomba Mahakama iamuru walipwe Sh500 milioni kama fidia na gharama ya
kesi.
- Mwananchi -
- Mwananchi -
Post a Comment