Mama ambaye hakuweza
kufahamika mara moja jina lake, akimrushia konde zito jamaa aliyedaiwa kumwibia
mkoba wake mama huyo, uliokuwa na pesa, simu pamoja na Paspoti ya kusafiria ya
mumewe anayeonekana pichani (wa pili kulia). Imeelezwa kuwa mama huyo alikuwa
amenasa katika kijimtaro eneo la Kituo cha Samaki Mbezi Beach jana usiku majira
ya saa nne, na kuamua kuomba msaada wa kunasuliwa gari yake katika eneo hilo
kutoka kwa waendesha Pikipiki 'Boda Boda' waliokuwa wakisubiri abiria kituoni
hapo.
Imeelezwa kuwa baada ya
kuoba msaada walijitokeza vijana kutoka miongoni mwa waendesha pikipiki hao na
kumnasua mama huyo wakisaidiana na mumewe, lakini baada tu ya kufanikisha zoezi
hilo mmoja wao aliingiza mkono katika dirisha la nyuma na kuchukua mkoba na
kisha kuanza kukimbia nao huku mume wa mama huyo akijitahidi kuwakimbiza bila
mafanikio, huku jamaa huyu aliyekamatwa akisikika kuwatetea jamaa hao, akisema,
'achana nao hao mimi nawafahamu', ndipo mume wa mama huyo alipoamua kuruachana
nao kwani walivuka barabara na kutokomea goizani upande wa pili wa barabara na
kurudi kuanza kumuuliza vizuri jamaa huyo ili waweze kufanya taratibu za
kuwapata.
Ghafla jamaa huyo alianza
kukana kuwa hawafamu, ndipo songombingo ilipoanza kwani mume na mke waliamua
kumng'ang'ania jamaa huyo huku wakisaidia na baadhi ya waendesha pikipiki
waliokuwa eneo hilo hadi walipofanikiwa kumpandisha katika gari yao na kuelekea
naye kituoni.
Shughuli ya kumdhibiti
ikiendelea.
Mama huyo akiendelea
kumdhibiti jamaa huyo kwa kumpiga tanganyika jeki.
Jamaa huyo naye akigeuka
mbogo huku akijaribu kujitetea na kuwa mkali bila
mafanikio.
credits: Sufiani Mafoto
credits: Sufiani Mafoto
Post a Comment