MAUAJI YA PADRI MUSHI: RIPOTI YA KAMISHNA WA POLISI ZANZIBAR...!!!
Kamishna wa Polisi Zanzibar
Mussa Ali.
Alisema kwa mujibu wa
taarifa kutoka kwa maafisa wa jeshi hilo Padri Mushi ,alipigwa risasi akiwa
kwenye ndani ya gari na kujeruhiwa vibaya sehemu za kichwa na
kifua.
Alisema baada ya kutokea
kwa tukio hilo punde baadhi ya waumini wa kanisa hilo waliofika katika kanisa
hilo kwa ajili ya ibada walimpeleka Padri Mushi katika hospitali kuu ya Mnazi
Mmoja kwa ajili ya matibabu baada ya muda mchache Akafariki
dunia.
Kutokana na uzito wa
tukio hili jeshi la polisi Zanzibar linaendelea na upelelezi wa kina kuhakikisha
wahusika wote wanafikishwa katika vyombo vya kisheria.”Alisema kamishna
Mussa
Hii ni gari aliyokuwamo
Padri Mushi.
Natoa wito kwa wananchi
washirikiane na maafisa wetu juu ya taarifa zozote zinazohusiana na tukio hili
ili tuweze kutekeleza majukumu kwa wakati.” Aliendelea
kusisitiza
Kamanda wa polisi mkoa
wa Mjini Magharibi Zanzibar ,ACP Aziz Mohamed alisema kwa sasa jeshi la polisi
linaendelea na doria katika maeneo mbalimbali ya Mjini wa Zanzibar ili
kuhakikisha wale wote wanaohusika katika mauaji ya padri huyo
wanakamatwa.
Wakati huo huo ,Naye
Mkuu wa Mkoa Mjini Magharib Abdallah Mwinyi Amefika katika Viunga vya Hospitali
ya Mnazi Mmoja Mnamo wa Saa 4 Asubuhi kwa ajili ya kuwafariji Jamaa,ndugu na
waumini wa dini hiyo waliofika katika eneo hilo kwa ajili ya kufuatilia hatima
ya kiongozi wao.
Akizungumzia tukio
hilo,msemaji wa kanisa hilo ambaye pia ni katibu mkuu wa kanisa katoliki,jimbo
la Zanzibar padri Cosmas Shayo aliwataka waumini wa kanisa hilo,kuwa wavumilivu
kwa kipindi hiki hadi suala hilo litakapotafutiwa
ufumbuzi.
Alisema Uongozi wa
kanisa hilo,umepokea suala hilo kwa masikitiko makubwa pia kufariki kwa padri
huyo ni miongoni mwa pigo kubwa kwa waumini na kanisa kwa
ujumla.
Tukio hili si la
kufumbia macho kwani viongozi na waumini wa kanisa katoliki Zanzibar kwasasa
tunaishi kwa mashaka hali ya kuwa,mtu ukitoka asubuhi huna uhakika wa kurudi
jioni ukiwa hai”Alisema padri Shayo.
Kwa nini matukio haya
yanaandama waumini na viongozi wa kanisa katoliki hapa kuna agenda ya siri hadi
tunafikia hatua ya kuishi kama watumwa tukiwa na hofu juu ya usalama wa maisha
yetu,serikali na vyombo vya ulinzi vikiwa vinakaa kimya.”Aliendelea kusema Padri
shayo.
Alisema Kanisa
linathamini mchango mkubwa uliotolewa na marehemu wakati wa uhai wake,katika
kuliendeleza kanisa kwenye huduma za kiimani na kiroho kwa waumini wa
kanisa.
Baadhi ya mashuhuda
,waliozungumza kwa nyakati tofauti katika eneo la tukio ambapo walisema kwamba
walifika mapema katika Kanisa hilo kwa ajili ya maandalizi ya ibada,pembeni mwa
kanisa hilo kulikuwa na watu watatu ambao hawakujulikana kwa haraka ghafla baada
ya kufika padri Mushi walisikia milio ya risasi wawili wakaondoka mbio na
pikipiki aina ya vespa na mmoja akatokomea Vichochoroni.
Padre Evaristus Mushi
ameuwawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana ambao walikua wamepanda
pikipiki aina ya Vespa leo asubuhi wakati akielekea kuongoza misa katika kanisa
la Mtakatifu Theresia la Beit el Rass.
Wananchi wamesikika wakitupia
lawama jeshi la polisi kwa kushindwa kudhibiti uharifu na umiliki wa silaha
kinyume cha sheria,kwani matukio ya kushambuliwa kwa viongozi wa dini mbalimbali
Zanzibar yameshamili.Wakati huo huo ,Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt,
Emmanuel Nchimbi amesema serikali itahakikisha inafanya juhudi kuhakikisha
inawakamata watu waliomuua Padre Evarist Mushi wa kanisa katoliki
Zanzibar.Akizungumza na waandishi wa habari huko Makao makuu ya
Polisi Zanzibar Dkt, Nchimbi amesema serikali imesikitishwa na tukio hilo
alilolieleza kuwa ni la kigaidi huku akishtumu kuwa wana lengo la kuingiza nchi
katika machafuko.
Amesema kuwa tukio hilo
si tukio la ujambazi bali tukio la kigaidi kwani limelenga zaidi katika
kuwashambulia viongozi kidini.
Amesema kuwa tukio hili
limefanana na tukio lililotokea mwishoni mwa mwaka jana la kushambuliwa kwa
risasi Padre Ambrose Mkenda wa Kanisa katoliki parokia ya
Mpendae
Amesema kuwa katika
kukabiliana na matukio ya kihalifu hapa nchini Wizara imeomba kibali kwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kushirikia na mashirika ya kimataifa ya
upelelezi ili kuwakamata wahalifu hao.
Dkt, Nchimbi amewataka
Watanzania kuwa wavumilivu na kujiepusha katika mtego wa kuchukia na kwa misingi
ya kidini katika kipindi hichi ambacho Jeshila Polisi linaendelea na upelelezi
wa tukio hilo.
Post a Comment