Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Dk. Emmanuel
Nchimbi (katikati) akiwa katika picha na Mbunge wa Uingereza, Lord Dholakia
(kushoto) pamoja na Ofisa wa Ubalozi wa Uingereza nchini, Julian Chandler.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Dk Emmanuel
Nchimbi (kulia) akifurahi jambo na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini,
Kamishna Jenerali John Minja wakati walipokuwa wanaenda sehemu ya chakula
hotelini hapo. Kushoto ni Ofisa wa Ubalozi wa Uingereza nchini, Julian
Chandler.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Dk Emmanuel
Nchimbi akizungumza na Mbunge wa Uingereza, Lord Dholakia (katikati),
ambaye amekuja nchini kwa ziara ya kikazi. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la
Magereza, Kamishna Jenerali John Minja. Waziri alibadilishana mawazo
na mbunge huyo katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, kuhusu
shughuli mbalimbali zinazofanywa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Dk Emmanuel
Nchimbi (wa tatu kutoka kulia) akizungumza na Mbunge wa Uingereza, Lord
Dholakia (wa pili kutoka kulia), na maofisa mbalimbali wa ubalozi wa
Uingereza nchini. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Magereza, Kamishna Jenerali
John Minja, wengine ni maofisa wa wizara hiyo.
Mbunge wa Uingereza, Lord Dholakia (wapili kutoka kulia) akizungumza katika
kikao hicho.
--
PICHA ZOTE
NA-FELIX MWAGARA
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
Post a Comment