Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MEYA MANISPAA KINONDONI AHAMASISHA USAFI WA MAZINGIRA WAKAZI WA MWANYAMALA


 

Wakazi wa Mtaa wa Kwa Msisiri A na Bwanwani, Kata ya Mwanayamala, Manispaa ya Kinondoni wakishirikiana na Meya wa Manispaa hiyo, Yusuph Mwenda, Diwani wa Kata hiyo, Songoro Mnyonge na Mkuu wa Wilaya hiyo, Jordan Rugimbana kufanya usafi katika Mtaa wa kwa Msisiri A, Dar es Salaam mwishoni ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya kuweka mazingira safi Manispaa hiyo mwishoni mwa wiki.
Diwani wa Kata ya Mwanayamala, Songoro Mnyonge akimpa maelezo Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuph Mwenda (wa tatu kulia) kuhusu mkakati wa kuboresha mtaro wa kupitisha majitaka uliopo katika Mtaa wa Bwawani, wakati wa mwendelezo wa kampeni ya kuweka mazingira safi Manispaa hiyo mwishoni mwa wiki. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Jordan Rugimbana na Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa, Mtaa wa Bwawani, Mohamed Mkandu (kulia).
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph mwenda (wa pili kushoto) akikagua ujenzi holela wa moja ya nyumba ya mkazi wa Mtaa wa Bwawani (kushoto), Kata ya Mwananyamala, Manispaa hiyo unaopelekea kujaa kwa madimbwi ya maji wakati wa zoezi la kuhamasisha uwekaji safi mazingira mwishoni mwa wiki ikiwa ni kampeni endelevu aliyoizindua hivi karibuni. Kushoto kwake ni Diwani wa Kata hiyo, Songoro Mnyonge na Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa, Mtaa wa Bwani, Mohamed Mkandu.
Wakazi wa Mtaa wa Kwa Msisiri A na Bwawani, Kata ya Mwananyamala, Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam wakizibua moja ya chemba za mitaro ya kupitishia majitaka wakati wa zoezi la uhamasishaji usafi wa mazingira lililoendeshwa na Meya wa Manispaa hiyo, Yusuph Mwenda, Mkuu wa Wilaya hiyo, Jordan Rugimbana na Diwani wa Kata hiyo, Songoro Mnyonge.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (kulia) akizungumza na viongozi na wakazi wa Kata ya Mwananyamala, Manispaa hiyo wakati wa zoezi endelevu la uhamasishaji usafi wa mazingira katika Kata hiyo lililofanyika mwishoni mwa wiki katika Kata hiyo.
Wakazi wa Mtaa wa Kwa Msisiri A na Bwawani, Kata ya Mwananyamala, Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam wakishhudia kijiko cha Manispaa hiyo kikizibua moja ya chemba za mitaro ya kupitishia majitaka wakati wa zoezi la uhamasishaji usafi wa mazingira lililoendeshwa na Meya wa Manispaa hiyo, Yusuph Mwenda, Mkuu wa Wilaya hiyo, Jordan Rugimbana na Diwani wa Kata hiyo, Songoro Mnyonge.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top