Na Waandishi Wetu
IWAPO Tanzania itafungiwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), au kutokea mgogoro wowote utakaoathiri soka ya nchi hii, basi Rais wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Leodegar Chilla Tenga ndiye atastahili kubeba lawama, imeelezwa.
Aidha, Tenga ametakiwa kuwaomba radhi wadau wa soka nchini kwa kuwa alikosea na kukiuka katiba ya TFF katika kufanya mabadiliko au marekebisho ya Katiba kwa kutoitisha Mkutano Mkuu amnbao una mamlaka ya kufanya mabadiliko ya katiba hiyo.
Hayo yamesemwa leo mjini Dar es Salaam na aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Makamu wa Rais wa TFF, Michael Richard Wambura alipozungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo).
Alisema kwa kuwa tayari serikali imeshatoa uamuzi wake kuhusiana na mustakabali mzima wa uchaguzi huo analazimika kuamini Tenga na kamati yake watatii na kutekeleza uamuzi huo na hasa ikizingatiwa kuwa ndani ya kamati hiyo kuna wajumbe ambao ni watumishi wa serikali.
Watumishi hao wa serikali ni pamoja na Athuman Nyamlani (Mahakama), Cresentius Magori (NSSF), Athumani Kambi (Tanroad) na Wallace Karia (TAMISEMI).
“Kwa kwenda kinyume na maamuzi ya serikali itakuwa ni utovu mkubwa wa nidhamu, hinyo napenda kuwasihi na kuwashauri ili wajipime na kujitathmini wakati wakijadili utekelezaji wa maamuzi ya Serikali,”alisema .
Wambura alienda mbali na kusema kwamba anashindwa kuelewa na kuamini msimamo wa Tenga kwani kama ni mtu mwenye kumbukumbu nzuri mwaka 2001 wakati anajiuzulu nafasi ya Makamu wa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) akiwa anzungumza na waandishi wa Habari march, 2001 alijaribu kuwaonesha Watanznia kuwa yeye ni muumini wa kufuata sheria na taratibu zilizopo.
“Hatuna budi kutekeleza majukumu yetu kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo kinyume chake ni vurugu, pale tunapoona sheria yetu inapitwa na wakati na haifai inatulazimu tukubaliane kuifanyia mabadiliko kabla hatujaacha kuiheshimu,”L.C Tenga (2001).
…hivyo ni wazi Tenga anafahjamu kuwa kwenda kinyume na utaratibu halali uliowekwa wa mabadiliko ya kAtiba ya TFF mwishowe huleta vurugu kama ambavyo Falasafa yake inavyomuelekeza, kwa mantiki hiyo anatulazimisha Watanzania kuamini mkanganyiko huu uliopo sasa Tenga anaufahamu mapema na alishiriki na kuruhusu hali hiyo itokee kwa msalahi yake binafsi,”alisema Wambura.
Wambura alisema Tenga katika mkutano wake na waandishi wa habari alieleza moja ya sababu za kujiuzulu kwake nafasi ya makamu Mwenyekiti wa BMT ni kupinga uamuzi wa serikali wa kukubaliana na FIFA kuhusu uundwaji wa kamati ya mpito ya FAT kwa madai kwa kufanya hivyo serikali itakuwa imepoteza uwezo wa kusimamia vyama vya michezo nchini.
…kukubali kutekeleza agizo la FIFA kama ilivyo amuliwa na serikali ni kuzitekeleza taratibu na sheria za nchi, serikali inajivua madaraka ya udhibiti wa vyma vya michezo vya kitaifa na kulikabidhi jukumu hilo kwa vyma vya michezo vya kimtaifa.Haiwezekani tufanye hivyo na hakuna nchi yoyote makini inayofanya hivyo”, Tenga 2001.
Kama hiyo haitoshi Wambura ameshauri baadhi ya mambo kwa kamati ya Utendaji kwa lengo la kunusuru soka la Tanzania kuingia katika mgogoro mpya, TFF iridhie kutekeleza uamauzi wa Serikali bila kigugumizi.
“TFF itangaze tarehe mpya na mchakato wa uchaguzi, pia kutokana na kuwepo kwa mashauri mawili katika mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza na Tanga, TFF ikutane na walalamikaji ili mashauri yamalizike nje ya mahakama kwani hata kama FIFA watakuja uchaguzi hauwezi kufanyika kwa kuwa tayari kuna zuyio la muda kusimamisha uchaguzi uliotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Tanzania”
“Ili haki itendeke wale wote walioomba na watakaooomba kugombea nafasi mbalimbali waruhusiwe na wapitishwe ili wapiga kura waamue kiongozi wanaomtaka, pia mabadiliko ya katika yangoje uongozi mpya utakaoingia madarakani ili nao waone na kuchambua mapungufu na kuyarekebisha,”
“Kwa kuwa kamati ya uchaguzi muda wake wa kukaa ofisini kikatiba ni miaka miwili ni wazi muda wao utakuwa umefikia ukomo ni vema ukaandaliwa utaratibu wa muda ili ipatikane kamati itakayosimamia uchaguzi huo, pia katika kuendesha na kusimamia uchaguzi huo kanuni za uchaguzi zilizotumika katika uchaguzi wa 2008 zitumike”
Wambura pia ameitaka kamati ya utendaji itoe tamko la kumuwajibiusha katibu mkuu wa TFF Angetile Osia kwa utovu wa nidhamu kwa kutoa matamshi ya kejeli dhidi ya waziri mwenye dhamana ya kusimaia michezo.
“Baada ya kufanya haya niliyoyapendekeza TFF iitaarifu FIFA kuwa Tanzania imetatua mgogoro wake yenyewe na hivyo kuiondoa katika orodha ya aibu ya nchi ambazo haziwezi kuandaa na kusimia chaguzi zake bila usimamizi wa FIFA,”aliongeza.
credits: Bin Zubeiry
Post a Comment