Katibu Tawala Mkoa Kagera wa Kwanza
Kushoto Bw. Nassor Mnambila Pamoja na Wawakilishi wa Mashirika ya UOA-T
na SAJAWAKA Kulia Wakijitayarisha Kuaini Mkataba wa Maelewano Katika
Kuendeleza Kituo cha Kutunza Wazee na Watoto Yatima Kiilima
Katibu Tawala Mkoa Kagera Bw. Nassor
Mnambila Akipena Mkono Peter B. Temalilwa Muwakilishi SAJAWAKA baada ya
Kuweka saini Katika Mkataba wa Maelewano.
Katibu Tawala Mkoa Kagera Bw. Nassor Mnambila Akisaini Mkataba wa Maelewano Kati ya UOA-T na SAJAWAKA.
Wazee na watoto yatima
wanaotunzwa katika kituo cha Kilima Halmashauri ya Wilaya Bukoba mkoani Kagera wapata ufadhili ili kuboreshewa
mazingira wanayoishi pia na huduma zote wanazostahili kupata katika umri wa uzee na watoto yatima.
Ufadhili
huo utapatikana baada ya Katibu Tawala Mkoa Kagera Bw. Nassor Mnambila
kutiliana saini katika Mkataba wa Maelewano
leo tarehe 12/02/2013 na mashirika
mawili yasiyokuwa ya serikali kuhudumia
kituo hicho kwa miaka mitano kwa pamoja yakishirikana na serikali.
Bw.
Mnambila amesaini mkataba huo kwa niaba ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
kwasababu kituo hicho kipo chini ya wizara hiyo, isipokuwa serikali ya mkoa wa
Kagera imehusika kusaini mkataba wa
maelewano kwaajilia ya ufuatiliaji wa karibu katika kituo hicho.
Mashirika
yaliyotiliana sahihi na serikali ya Mkoa ni UKIMWI Orphans Assistance (UOA),
U.S.A, P.O.Box 29074 Washington, DC 20017 kupitia UKIMWI Orphans Assistance -
Tanzania (UOA-T), P.O. Box 1074 Bukoba, shirika hilo litashirikiana na Saidia
Jamii ya Wazee Kagera (SAJAWAKA) P.O.Box 603 Bukoba.
Katika
mkataba huo wa maelewano mashirika
yasiyokuwa ya kiserikali yatahusika na kukarabati miundombinu ya kituo hicho cha
Wazee na Watoto yatima ambayo ni pamoja na mabweni, bafu, nyumba za watumishi,
jiko, stoo na bwalo la chakula na kuweka samani ndani ya majengo hayo.
Aidha
pamoja na kushirikiana na mashirika hayo, serikali itaendelea kuhakikisha utulivu na amani katika kituo
hicho. Pia serikali itaendelea kutoa huduma zilizokuwa zikitolewa hapo mwanzo
kama mishahara ya watumishi wa kituo hicho na huduma nyingine kama chakula
ilizokuwa ikizitoa tangu awali.
Matarajio ya Baadae, Serikali katika kuongeza ushirikiano
wa kutoa huduma za kijamii kwa kushirikiana na Sekta binafsi (Public and
Private Partnership, PPP) inatarajia kujenga dispensari katika kituo hicho ili
kuhudumia wazee, watoto yatima pamoja na jamii ya Kilima.
Kuhakikisha
kituo hicho kinajiendesha kwa kutegemea kilimo na kupata chakula cha kutosha
kukidhi mahitaji ya kituo. Pia kukisaidia kituo hicho kunufaika na rasilimali zinazotarajiwa
kupatikana katika kituo hicho.
Kituo
cha Kiliima kinatarajiwa kufanywa kituo cha mafunzo kwa vitendi kwa wanafunzi
wa elimu ya kijamii na Afya ambao watajifunza
kwa vitendo kuwatunza wazee na watoto yatima na baadae kuajiliwa katika sehemu mbalimbali za Tanzania kuwatunza wazee na watoto.
Kituo
cha Kiilima Kilianzishwa mwaka 1972 na serikali ya Tanzania chini ya Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii kwajili ya
kuwatunza wazee na watoto yatima. Aidha
Shirika la UOA-U.S.A/UOA-T, ni kati ya mashirika yasiyokuwa ya serikali na
limefanya kazi mkoani Kagera kwa miaka 23, pia SAJAWAKA limefanya kazi mkoani Kagera kwa
miaka 12.
Hili ni jengo Mojawapo Katika
Kituo cha Kuwatunza Wazee na Watoto Yatima Liloezuliwa na Upepo na
Kuwafanya Wazee wa Kiilima Kubakia na JengoMoja.
Bibi Huyu ni Mmojawapo Kati ya Wazee Wanaotunzwa Kituoni Kiilima Katika Halmashauri ya Wilaya Bukoba.
Credits: Bukoba Wadau
Post a Comment