|
Zainabu
Zuberi mwenye kitambaa cheusi kichwani akiongozana na askari kanzu pamoja na
waandishi wa habari mara baada ya kuokolewa na askari hao eneo la tukio ili
asishambuliwe na wananchi wenye hasira kali wakimtuhumu kuwa ni
mchawi
|
|
Zainabu
Zuberi akituhumiwa kuhusika na
ushirikina.
|
|
Mume
wa Mtuhumiwa huyo Sulemani Rubea(49) amekataa mke wake kutuhumiwa kwa ushirikina
ambapo aliwatupia lawama wanakijiji kwa madai kuwa wanaendekeza udini na
kutopenda maendeleo na ndiyo maana hawawataki mtaani
hapo.
|
|
Moja
ya askari akipata maelezo kwa mama aliyepotelewa na mtoto wake katika mazingira
ya kutatanisha wiki mbili zilizopita mpaka sasa hajapatikana mtoto
huyo |
|
Wananchi
hao kwa pamoja waliazimia kumhamisha Mwanamke huyo Mtaani hapo katika mkutano
ulihudhuriwa na wakazi zaidi ya 200 ambao walidai kuchoshwa na hali
hiyo.
|
|
Hii
ndiyo nyumba anayoishi anaetuhumiwa kwa uchawi ilolo
Mbeya |
|
Mwenyekiti wa Mtaa wa Ilolo Kati Ngambi Kulaba
Ngambi amesema wananchi walikuwa wakimtuhumu yeye kuwa anamlinda mwanamke huyo
ili aendelee kuishi mtaani pale ili hali wao hawamtaki mtaani hapo.
Wananchi wa Mtaa wa Ilolo Kata ya Manga Jijini humo
kumfukuza mtaani hapo Mwanamke anaye fahamika kwa jina la Zainabu Zuberi
akituhumiwa kuhusika na ushirikina.
Wananchi hao ambao
awali walitaka kujichukulia hatua mkononi kwa kumpiga na kumchomea moto nyumba
yake mtuhumiwa huyo walidai kuchoshwa na maovu yanayofanywa na mwanamke
huyo.
Baadhi ya matendo ya
kishirikina wanayomtuhumu mwanamke huyo kuhusika nayo ni pamoja na kujigamba
kuwamaliza wanakijiji hao kwa kuwaloga ikiwa ni pamoja na kuwaloga watoto wao
kitu ambacho wanasema kimeshatokea.
Wamedai kuwa mwanamke
huyo amekuwa akiwagusa wanawake wajawazito na mimba zao huharibika ambapo pia
wanafunzi wanaotoka katika mtaa huo wakifika Shule hushindwa kuona kabisa
matukio ambayo mwanamke huyo anahusishwa.
Walisema mwanamke huyo
anatuhumiwa kujihusisha na matukio ya kishirikina tangu ahamie mtaani hapo
takribani miaka mitatu ambapo walisema wakazi hao walimwonya mapema kuhusu tabia
hiyo baada ya kufuatilia historia ya maeneo aliyowahi
kuishi.
Kwa upande wake Mume wa
Mtuhumiwa huyo Sulemani Rubea(49) amekataa mke wake kutuhumiwa kwa ushirikina
ambapo aliwatupia lawama wanakijiji kwa madai kuwa wanaendekeza udini na
kutopenda maendeleo na ndiyo maana hawawataki mtaani
hapo.
Rubea ameongeza kuwa
mtaani hapo hawapendi mtu wa dini ya nyingine kujenga eneo hilo jambo ambalo
lilipingwa vikali na wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara uliokuwa na lengo
la kumjadili mtuhumiwa huyo.
Awali mume wa mtuhumiwa
huyo alikiri kuhama nyumba na mitaa zaidi ya kumi ambapo lisema maeneo mengine
alikuwa amejenga lakini sehemunyingine alikuwa amepanga tu ingawa aligoma kusema
sabbu inayomfanya ahame maeneo hayo.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa Mtaa wa Ilolo Kati Ngambi Kulaba Ngambi amesema wananchi walikuwa
wakimtuhumu yeye kuwa anamlinda mwanamke huyo ili aendelee kuishi mtaani pale
ili hali wao hawamtaki mtaani hapo.
Amesema baada ya kuona
wanachi wamepagawa na kutaka kujichukulia hatua mkononi ili mlazimu kuitisha
mkutano wa hadhara ikiwa na kuitaarifu jeshi la polisi ambalo lilifika mapema
eneo la Mkutano na kwatuliza wananchi wasifanye lolote ambapo Askari hao
waliondoka na mtuhumiwa.
Aidha katika mkutano
huo wananchi hao kwa pamoja waliazimia kumhamisha Mwanamke huyo Mtaani hapo
katika mkutano ulihudhuriwa na wakazi zaidi ya 200 ambao walidai kuchoshwa na
hali hiyo.
Matukio kama hayo
yanayoashiria vitendo vya kishirikina ni pamoja na tukio la hivi karibuni la
watu wawili kuzikwa wakiwa hai wakituhumiwa kuhusika na vitendo hivyo viovu
ndani ya jamii.
Na Mbeya
yetu
|
on Monday, February 11, 2013
Post a Comment