Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MWENYEKITI WA CCM RAIS DK. JAKAYA KIKWETE AWAONGOZA MAADHIMISHO YA MIAKA 36 YA CCM


22Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dk. Jakaya Kikwete akihutubia wananchi katika sherehe za miaka 36 ya CCM zilizofanyika jioni ya leo kwenye uwanja wa Lake Tanganyika Mkoani Kigoma na kuhudhuriwa  na wananchi mbalimbali waliojitokeza kushiriki katika sherehe hizo.
Wawakilishi wa vyama rafiki vya CCM kutoka nchini Burundi CNDD kinachotawala nchini humo, na PPRD kinachotawala nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
16Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana akizungumza katika maadhimisho hayo.
23Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe akizungumzia mikakati ya Serikali katika maadhimisho hayo juu ya urejeshaji wa huduma za treni katika kituo cha Reli ya Kati cha Kigoma.
14Kikundi cha ngoma kutoka nchini Burundi kikitumuiza katika maadhimisho hayo yaliyofanyika leo kwenye uwanja wa Lake Tanganyika.
15Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza katika maadhimisho hayo katika uwanja wa Lake Taganyika.
2Rais Jakaya Kikwete akiangalia picha zilizochorwa zikimuonesha yeye na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere wakati alipotembelea mabanda ya maonyesho katika maadhimisho ya miaka 36 ya CCM
5Rais Jakaya Kikwete akiangalia ndizi zinazozalishwa mkoani Kigoma katika banda la wakulima wa ndizi kutoka mkoa huo.
6Rais Jakaya Kikwete akiwapungia mkono wananchi wa mkoa wa Kigoma waliojitokeza kwenye maadhimisho ya miaka 36 ya CCM kwenye uwanja wa Lake Tanganyika.
7Wananchi mbalimbali wakiwa wamejitokeza kwenye uwanja wa Lake Tanganyika.
8Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimtunza mmoja wa wasanii wadogo wa kikundi cha ngoma kutoka nchini Burundi kilichoshiriki katika maadhimisho ya miaka 36 ya CCM.
9Rais Jakaya Kikwete akiangalia vikundi vya ngoma mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Lake Tanganyika kwa ajili ya kushiriki katika maadhimisho ya miaka 36 ya Chama Cha Mapinduzi CCM  Kutoka kushoto ni Makamu Mweyekiti Bara Mzee Philip Mangula, Naibu Katibu Mkuu Bara Mwigulu Nchemba na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana.
10Wananchi wakiwa wamefurika kwenye uwanja wa Lake Tanganyika.
11Vijana wa Chipukizi wa CCM wakipita kwa Gwaride la Heshima na Utii mbele ya Rais Jakaya Kikwete.
13Vijana wa Chipukizi wakiimba wimbo wa Kwaya katika maadhimisho hayo.
18Msanii Diamond akiongoza kundi lake katika kutoa burudani kwa wananchi waliojitokeza katika maadhimisho hayo.
20Mwanamuziki Diamond akiwaburudisha wananchi kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma katika maadhimisho ya miaka 36 ya CCM mjini Kigoma leo.
SOURCE FULL SHANGWE
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top