Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Kassim Majaliwa (Mb),
akizungumza na walimu wakuu wa shule za sekondari mkoa wa Singida na baadhi ya
watendaji wa sekta ya elimu. Mazungumzo hayo ambayo yalikuwa ni pamoja na kuweka
mikakati ya kuinua taaluma mkoani Singida yamefanyika kwenye ukumbi wa mikutano
wa ofisi ya mkuu wa mkoa mjini Singida. Kushoto ni kaimu mkuu wa mkoa wa Singida
ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Ikungi, Manju Msambya na Kulia ni katibu tawala
mkoa wa Singida, Liana Hassan.
Baadhi ya walimu wakuu wa
shule za sekondari mkoa wa Singida wakimsikiliza kwa makini Mh. Kassim Majaliwa
(hayupo kwenye picha). (Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel
Limu.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Kassim Majaliwa,
amesema kuanzia sasa kazi ya kuandikisha wanafunzi kuanza madarasa ya awali na
yale ya msingi, itafanywa na watendaji wa vijiji na si walimu wakuu wa shule za
msingi.
Majaliwa amesema hayo
wakati akizungumza na walimu wakuu wa shule za sekondari na baadhi ya viongozi
wa sekta ya elimu mkoani Singida.
Amesema kutokana na ukweli
huo, serikali itafanya kazi ya uandikishaji watoto wenye sifa ya kuanza
madarasa ya awali na yale ya msingi, ni watendaji wa vijiji na kazi hiyo,
itakuwa na ufanisi mkubwa kuliko kipindi cha miaka ya
nyuma.
Aidha, Naibu Waziri huyo
amesema kuwa kila mtendaji wa kijiji anapaswa kuwakilisha ripoti ya kazi ya
uandikishaji wanafunzi wa shule za awali na wale wa msingi mbele ya kikao cha
maendeleo ya kata (WDC) ili kupata Baraka ya kikao hicho.
Majaliwaa mesema ili kuipa
umuhimu mkubwa elimu ya awali ni lazima kuwepo na bajeti ambazo zitaonyesha
ongezeko la shule za awali.
Katika hatuna nyingine,
Naibu Waziri huyo amekumbusha kuwa kila shule ya msingi ni lazima iwe na vyumba
vya kutosha vya madarasa ya awali.
Mh. Majaliwa amesema
wanafunzi wa shule za awali sio walundikwe tu madarasani au wawe wa kucheza tu
kipindi chote wawapo shuleni, hapana, ihakikishwe wanasoma kikamilifu ili
wakianza darasa la kwanza katika shule za msingi, wawe wameiva
barabara.
Post a Comment