|
Katibu wa
NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimkabidhi cheti Ndugu Leonard Ismail
Suleiman Kitwara,Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi CCM,tawi la Ofisi Ndogo,Makao
Makuu Lumumba katika sherehe za ufunguzi wa ofisi za Tawi.
**********
Chama Cha Mapinduzi-CCM-kimesema kina
uhakika wa kushinda katika Uchaguzi Mkuu ujayo wa mwaka 2015 kutokana na kwamba
bado kipo imara na kinakubalika na Watanzania wengi.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar
es salaam na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Ndugu NAPE NNAUYE wakati
akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Tawi la Ofisi Ndogo Makao Makuu na
baadhi ya wanachama wa Tawi hilo mara baada ya kufungua Ofisi Mpya ya Tawi la
Ofisi Ndogo.
Kwa imani hiyo amesema hakuna sababu ya
Wana-CCM kukata tamaa kwani wamezunguka Mikoani na kujionea hali halisi ya jinsi
wananchi wanavyoendelea kukiamini Chama tawala ambacho ni Chama cha Wakulima na
Wanyonge.
Kuhusu migongano ya Dini Katibu huyo
wa NEC, Itikadi na Uenezi amesisitiza kuwa migongano hiyo itamalizwa na Chama
kwa kushirikiana na viongozi na wananchi kwani CCM ndicho Chama pekee chenye
kudumisha amani na mshikamano miongoni mwa Watanzania.
Mapema akisoma risala ya wanachama wa
Tawi la CCM la Ofisi Ndogo ya Makao Makuu lililopo katika Kata ya Jangwani,
Katibu wa Tawi Ndugu ROSE THOMAS amesifu hatua mbalimbali zinazochukuliwa na
chama katika kurejesha imani ya CCM kwa wananchi.
Tawi
hilo la Ofisi Ndogo lina Mashina Sita na lina wanachama 308.
|
on Wednesday, February 20, 2013
Post a Comment