Ikiwa bado tuna majonzi ya kufiwa na mtumishi wa mungu
Padri Evarist Mushi huko Zanzibar,jana usiku watu wasiojulikana wamelishambulia kwa mawe
kanisa na baadae kulichoma moto kanisa la Walokole la Shaloom lililoko Kiyanga
kwa Sheha mkoa wa kusini Unguja Zanzibar.
Kamanda wa polisi mkoa wa kusini Unguja Agustino Ulomi
amesema hilo tukio limetokea jana saa tisa na nusu usiku, ambapo huo moto
ulianza kuwaka baada ya vijana watatu walioonekana karibu na kanisa, baadae
kidogo ndio mlinzi akaanza kusikia mawe yakirushwa juu ya bati.
Baada ya mlinzi kuona hatari ilibidi akajifiche lakini
kwa mbali akawa anaona kinachoendelea, moto ukiendelea ndio akampigia simu
kiongozi wa kanisa ambae aliwapigia polisi, wakaja wakawa wanashirikiana na
wananchi kuuzima japo tayari ulikua umeshaunguza samani mbalimbali za kanisa
hilo, kilichosaidia kanisa hilo kutoungua lote ni vifaa imara vilivyotumika
kulijenga.
Katika ripoti hii ambayo imeripotiwa na mwandishi wa
habari Cathbert Kajuna wa kajunason.blogspot.com bado hajakamatwa mtu yeyote mpaka
sasa, polisi wamesema pia wanaanza utaratibu wa ulinzi wa makanisa kutokana na
vitisho vilivyopo sasa hivi.
Habari za kina zinasema hakuna aliye jeruhiwa hata
mmoja lilotokea saa tisa ya usiku,usiku
wa kuamkia leo.
Post a Comment