Waziri wa Ardhi,Nyumba
na Maendeleo ya Makazi,Profesa Anna Tibaijuka akikata utepe wakati wa uzinduzi
wa hoteli mpya yenye hadhi ya nyota 4 ya palace jijini Arusha jana.Wanaoshuhudia
ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mh. Lazaro Nyalandu,Mkurugenzi Mkuu wa
NHC,Bw. Nehemia Mchechu na kulia mmiliki wa hoteli hiyo Dr.Hans
Macha.
waziri wa ardhi nyumba
na maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka akiangalia jiwe la msingi baada ya
uzinduzi wa hotel yenye hadhi ya nyota 4 Palace hoteli iliyopo katikati ya jiji
la Arusha.
WAZIRI wa ardhi nyumba
na maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka akikata keki yenye taswira ya
jengo la hotel ya palace pamoja na mke wa mkurugenzi mkuu wa Palace hotel Bibi
Vaileth ,Macha wakati wa uzindizi rasmi wa hoteli hiyo.
WAZIRI wa ardhi nyumba
na maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka,naibu waziri wa maliasili na
utalii Lazaro Nyalandu,Waheshimiwa Wabunge wa Majimbo ya Arusha na Arumeru
Mashariki,Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Nyumba na Mkutugenzi Mkuu wa
Hoteli hiyo waliongozana kuingia ndani ya jengo la hoteli hiyo.
WAJASIRIAMALI nchini,
wametakiwa kujitokeza katika ujenzi wa hoteli za kitalii nchini, ili kukabiliana
na tatizo kubwa la uhaba wa vitanda katika hoteli za kitalii ambao unalikabili
Taifa. Naibu waziri wa Maliasilia na Utalii, Lazaro Nyarandu, alitoa wito huo
jana wakati wa uzinduzi wa hoteli ya kitalii ya Palace Hoteli, ambayo imejengwa
kwa ubia na Shirika la nyumba nchini(NHC).
Lazaro alisema
uwekezaji huo utasadia kuongeza idadi kubwa ya watalii na mapato,”mwaka jana
tulipata watalii 800,000 ukilinganisha na nchi ya Rwanda na udogo wake ilipata
wageni 600,000 tatizo kubwa la nchi yetu ni upungufu wa vyumba vya kulala
wageni”alisema.
Alisema mkakati huo
utaufanya mkoa wa Arusha ambao ni kitovu cha utalii kuzidi kuongeza idadi ya
vitanda vya kisasa kulala wageni ambapo kwa sasa ina vitanda 2,800 tu nyuma ya
mkoa wa Dar es salaam wenye vitanda 3,800 na kuzidi mkoa wa Mwanza wenye vitanda
900 licha ya ukubwa wake.
“Tunaomba shirika la
nyumba lijitanue hadi maeneo hasa ujenzi wa hoteli za kisasa za kitalii…na sisi
wizara tunahitaji wawekezaji wa ndani na nje kujitokeza kujenga katika maeneo ya
wazi na ndani ya hifadhi zetu panapofaa…na tumejipanga kukabiliana na watumishi
wenye urasimu wanaokwamisha watu wenye nia njema”alisisitiza.
Awali Mkurugenzi Mkuu
wa NHC, Nehemia Mchechu alisema ujenzi wa hoteli hiyo yenye hadhi ya nyota nne,
umegharimu kiasi cha sh 16 bilioni ambapo NHC imetoa ardhi n ash 9 bilioni huku
kiasi kingine kikitolewa na Palace Hoteli.
Alisema mradi wa hoteli
hiyo ni moja ya miradi ambayo imekuwa na manufaa makubwa, kutokana na uwazi
katika uendeshwaji wake na hivyo kuingiza mapato kwa pande zote NHC na Mbia.
“binafsi nampongeza sana Mkurugenzi wa Palace hoteli, Dk Hans Macha kwa uwazi
katika uendeshwaji wa mradi huu na tunamkaribisha katika miradi mingine aje
tushirikiane”alisema Mchechu.
Naye Dk Ha Macha alisema
mradi huo hadi sasa imetoa ajira ya wafanyakazi 120 na unatoa huduma nyingine
kadhaa, ikiwepo huduma za kibenki na utachangia kwa kiasi kikubwa kikuza uchumi
wa mkoa wa Arusha na Taifa.
“hoteli hii tunatumia
malighafi za hapa Arusha toka kwa wajasiriamali ikiwa ni njia ya kuongeza ajira
na kipato na pia tumekuwa na miradi mbali mbali ikiwepo na utunzwaji wa
mazingira”alisema Macha.
Akifungua mradi huo
rasmi, Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alipongeza mradi huo na kutoa
wito kwa wajasiriamali wengine kujitokeza na kuingia ubia na NHC katika
kutekeleza miradi mbali mbali. Alisema mradi huo unakwenda vizuri na umeongeza
mapato ya NHC kwani katika eneo hilo, kabla ya ujenzi wa hoteli walikuwa
wakipata kwa mwaka kiasi cha sh 31 milioni pekee lakini sasa wanapata 151
milioni.
“natoa agizo rasmi kwa
wabia wengine walioingia mikataba na NHC kama huu, kama hawajatekeleza hadi sasa
basi mikataba yao ifutwe kwani ni hasara kwa shirika la Taifa”alisema Profesa
Tibaijuka.
Picha na Michuzi Blog
Picha na Michuzi Blog
Post a Comment