NAIBU Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele amesema kuwa serikali
haijatoa leseni ya uchimbaji madini ya urani kwa ajili ya Mto Mkuju.
Masele alitoa kauli hiyo wakati akijibu swali la Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), ambaye alitaka kujua kama ni kweli Serikali imetoa leseni ya uchimbaji kwa mradi wa Mkuju na kama ndiyo, alitaka kufahamu kama leseni hiyo imezingatia matakwa ya kisheria.
Mbunge huyo pia alihoji juu ya leseni mpya iliyotolewa ya North Mara Gold Mines Ltd kama imezingatia matakwa ya sheria mpya ya madini.
Akijibu maswali hayo kwa pamoja Naibu Waziri alisema kuwa kulingana na matakwa ya kisheria, uhuishaji wa leseni hizo umezingatia kukamilika kwa mchakato wa mazingira ya leseni ambazo zilitolewa kwa kipindi cha miaka 15.
Alisema iwapo kampuni itagundua mashapo zaidi siku za usoni baada ya muda huo, itabidi iombe tena kuhuishwa kwa leseni kwa ajili ya mgodi huo kuweza kuendelea na uchimbaji.
Kuhusu huduma za kijamii, Naibu Waziri alisema kuwa tangu mwezi Mei mwaka jana, migodi imefanya kazi kubwa ya kuboresha mazingira mazuri ya wananchi wanaozunguka migodi hiyo ikiwemo kuwaboreshea vyanzo vya maji.
TANZANIA DAIMA

Post a Comment