TAHADHARI KUHUSU WATU WANAO FANYA UTAPELI MTANDAONI
KWA JINA LA TAASISI YA RAFIKI ELIMU.
Uongozi wa Taasisi Ya
RafikiElimu Foundation unapenda kuwahadharisha wananchi wote juu
ya kuibuka kwa kundi la watu wanaofanya utapeli mitandaoni kwa kutumia
jina la Taasisi ya RafikiElimu ( RafikiElimu Foundation.)
Siku ya
Ijumaa ya leo tarehe 28 FEBRUARI 2013 mnamo
majira ya
saa 5 kamili asubuhi, ofisi yetu ilitembelewa na mwanadada aliye
jitambulisha kwa jina la HAWA MUSSA.
Mwanadada huyu
baada ya kujitambulisha, aliomba kuonana na HUMAN RESOURCES
MANAGER wa Taasisi ya RafikiElimu, baada ya kumuona alionesha
fomu aliyopewa kupitia mtandaoni na watu waliojitambulisha kwake
kama RafikiElimu Foundation.
Watu hao walitoa tangazo
kupitia mtandao wa ZOOM TANZANIA wakidai kuwa wana wa- link,
wahitimu mbalimbali wa vyuo vikuu na taasisi mbalimbali zisizokuwa
za kiserikali kwa ajili ya kufanya kazi katika taasisi hizo
kama volunteers.
Mwanadada huyu akaendelea kueleza ya
kwamba, baada ya kuona tangazo hilo alivutiwa na kutuma maombi ambapo
walimjibu kwa kumpatia fomu aliyo takiwa kuijaza na kuirejesha kwao.
Baada ya kujaza fomu hiyo, walimtumia barua pepe nyingine na kumwambia
kwamba maombi yake yamekubaliwa, kisha wakamtumia fomu na kumwambia
aijaze, aimbatanishe na CV yake, na kuwatumia pesa kiasi cha shilingi
Elfu Tano ( TSh. 5,000/=) kwa njia ya MPESA kwenda
namba 0763906931 (AMBAYO MBAYA ZAIDI, WAMEISAJILI KWA JINA
LA RAFIKIELIMU).
Baada ya kuwatumia pesa hiyo, wakamwambia
aripoti na fomu yake iliyojazwa na kuambatanishwa na CV kwa HUMAN
RESOURCES MANAGER wa Taasisi ya RafikiElimu (ambaye kwenye barua hiyo
walimtaja kama Mr. ALBERT EMMANUEL ) siku ya tarehe 28 FEBRUARI 2013
saa 5 kamili asubuhi.
Sisi Taasisi ya RafikiElimu tumeshangazwa
sana na taarifa hii kwa sababu kwanza, hatukutoa tangazo la aina hiyo,
lakini pili huwa hatuwatozi watu pesa ili kuwatafutia nafasi za
kujitolea. Tumefadhaishwa sana.
Tumebaini kuwepo kwa utapeli
unaofanywa na watu kwa jina letu, hivyo moja kwa moja tumekwenda
kuripoti tukio hili la uhalifu katika kituo kidogo cha polisi
kilichopo katika Chuo Kikuu Cha Dar Es salaam, sehemu ya Mlimani na
kupewa RB namba UD/RB/849/2013 WIZI KWA NJIA YA
MTANDAO. Tumelitazama tangazo hilo katika mtandao wa Zoom
Tanzania. Tangazo hili lililowekwa mtandaoni mnamo siku ya
tarehe 05 FEBRUARI 2013 lilisomeka kama ifuatavyo
:
UDHAIFU
WA TANGAZO HILI:
i. Namba waliyo weka haipo ( IT DOES NOT EXIST
)
ii. Wanasema " We are looking for Highly motivated individuals to
volunteer in differentprivate Organisation... (RafikiElimu
Foundation, hatushughuliki na private organizations bali NON-GOVERNMENTAL
ORGANIZATIONS).
iii. Namba za simu walizo weka, hazipo kwenye blogu
yetu.
iv. Katika tangazo lao, hakuna link inayo onyesha anuani ya
blogu yetu.
v. Wametoa tangazo lao kwa lugha ya kiingereza, sisi
kama RafikiElimu Foundation hatujawahi kutoa tangazo kwa lugha ya
kiingereza.
vi. Kiingereza walicho tumia ni kibovu sana.
vii.
Anuani ya barua pepe waliyo tumia ni batili na wala haipo kwenye
taarifa zetu za kwenye blogu yetu. Anwani ya barua pepe waliyo
tumia ni : graduatevolunteer@gmail.com wakati
anuani ya barua pepe ya taasisi ya RafikiElimu Foundation ni
: rafikielimutanzania@gmail.com
HATUA TULIYO
CHUKUA BAADA YA KULIONA TANGAZO HILI NI KUUFAHAMISHA UONGOZI WA
MTANDAO WA ZOOM TANZANIA, KUHUSU TANGAZO HILO LA KITAPELI ILI
KUWANUSURU WANANCHI WENGINE ZAIDI NA TUNASHUKURU ZOOM TANZANIA
WAMEPOKEA TAARIFA YETU NA KUAHIDI KULISHUGHULIKIA TATIZO HILO KWA
KULIONDOA KATIKA TOVUTI YAO .
UDHAIFU WA FOMU HII :
1. Namba zao
walizo zitoa kwenye fomu hizi za kitapeli, hazipatikani muda wote,
wakati namba zetu zinapatikana muda wote.
2. Katika fomu yao ya
kitapeli, hawajaandika location ya ofisi zilipo, hawajaweka sanduku la
barua, blog adress wala namba za simu zinazo patikana.
3. Hakuna
logo.
4. Hakuna sahihi.
5. Hakuna jina
6. Hakuna
muhuri.
Tulipo jaribu kuwapigia kwa namba walizo ziweka kwenye
mtandao ambazo ni +255 22 524 3785 tukajibiwa ya
kwamba namba hizo hazipo ( the number your dialing are not existing
).
Na tulipo jaribu kuwapigia kwa
namba 0763906931 nazo zikawa hazipatikani muda
wote.
Taasisi yangu kwa kushirikiana na jeshi la polisi,
tunafanya msako mkali dhidi ya mtu ama watu hawa na tunaahidi ya
kwamba tutawakamata ndani ya muda ambao si mrefu sana na kuwafikisha
kwenye vyombo vya dola.
OMBI: Kama na wewe ni
miongoni mwa walio tapeliwa na watu hawa, tafadhali wasiliana nasi kwa
simu 0782405936 ili tushirikiane katika kuhakikisha
wahalifu hawa wanatiwa mbaroni na kufikishwa katika vyombo vya
sheria.
TAMKO LETU : Tunalaani vikali kitendo kilicho
fanywa na ama kinacho fanywa na wahalifu hawa, kwani mbali na kuiba
pesa za Watanzania masikini kama wao, kitendo hiki kinachafua jina la
Taasisi yetu ambayo inafanya kazi zake kwa kushirikiana na
wananchi.
ANGALIZO KWA WANAOTAFUTA KAZI :
i. Unapo
tuma maombi ya kazi katika sehemu yoyote ile halafu ukaambiwa utume
pesa ili kupatiwa kazi hiyo, jua kwamba huo ni utapeli na kazi
hiyo haipo.
ii. Hakikisha unazifahamu ofisi za taasisi hiyo
zilipo kabla ya kuchukua maamuzi yoyote yanayo husisha
pesa.
iiii. Ni vyema kufanya uchunguzi ili kujiridhisha kama
taasisi hiyo kweli ipo.
iv. Unapoona tangazo la kazi, na kuvutiwa
nalo, jitaidi kuwapigia simu walioweka tangazo na kuwauliza maswali
mawili matatu kuhusu kazi hiyo.
HATA HIVYO: Tunashukuru kuwa mpaka
sasa ni mtu mmoja tu ndie aliyeripoti kutapeliwa na watu hao kwa
jina la Taasisi yetu. Hii ina maana kuwa Watanzania wengi wameelimika
kwa sasa, inawezekana watu wengine walilishitukia tangazo hili na
kuachana nalo.
Post a Comment