Rais wa TALISS
Swimming Club Bi. Najat Saleh Ahmed (mwenye miwani nyeusi) akizungumza
na washiriki pamoja na wageni waalikwa wakati wa ufunguzi wa mashindano
ya kuogelea yaliyoshirikisha Club mbalimbali na kwa rika tofauti
yaliyodhaminiwa na Kampuni ya CFAO Motors wauzaji wa magari ya kisasa
hapa nchini yaliyofanyika katika bwawa la kuogelea la shule ya Kimataifa
ya Tanganyika (IST). Amesema Mashindano hayo hufanyika kila mwaka na
kushirikisha vilabu na watu binafsi wenye ujuzi wa kuogelea unaofikia
kiwango cha kushiriki mashindano. Aidha Bi. Najat Ahmed ameomba wadau
zaidi kujitokeza kudhamini mashindano hayo na kuiomba Serikali ijitokeze
na kujenga mabwawa yanayohitajika kwa ajili ya watu kujifunza kuogelea
ili kuweza kujiokoa katika ajali za majini.
Pichani juu na chini washiriki wa club mbalimbali za kuogelea wakipita mbele wazazi na makocha kwa ajili ya utambulisho.
Official wakijipanga tayari kuanza mashindano hayo yaliyohusisha Clubs mbalimbali kutoka sehemu tofauti.
Pichani juu na chini
ni washiriki wajitosa kwenye bwawa hilo kuchuana katika mashindano ya
kuogelea yaliyoratibiwa na TALISS Swim Club na kudhaminiwa na kampuni ya
CFAO Motors ya jijini Dar.
Picha juu na chini
Sehemu ya watazamaji wakishuhudia mashindano hayo yaliyofanyika mwishoni
mwa wiki jijini Dar es Salaam katika shule ya Kimataifa ya Tanganyika
(IST).
Picha juu na chini
Meneja Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmed akiwavalisha medali washindi
wa mashindano hayo katika kategori mbalimbali. CFAO Motors imeamua
kudhamini mashindano hayo baada ya kuona umuhimu wa vijana kujua
kuogelea ili kuweza kujiokoa katika majanga yanayohusiha ajali za majini
zinazopelekea vifo vya watoto ikiwa ndio lengo la TALISS.
Rais wa TALISS
Swimming Club Bi. Najat Saleh Ahmed akikabidhi medali kwa mmoja wa
washindi wa mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Kampuni ya CFAO Motors.
Picha juu na chini
ni Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni ya CFAO Motors Wayne Mcintosh
ambaye pia alikuwa MC katika mashindano hayo akikabidhi vikombe kwa
washindi wa jumla walioshiriki TALISS Swimming Championships 2013.
Umati wa watu
wakiwemo wazazi, ndugu na jamaa pamoja makocha waliohudhuria kushuhudia
mashindano ya kuogelea ya TALISS yaliyohusisha vilabu kutoka sehemu
mbalimbali.
Pichani juu na chini
baadhi ya wageni waliohudhuria kutazama mashindano ya kuogelea katika
shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST) wakikagua gari mpya aina ya
Nissan Y62 inayosambazwa na Kampuni ya CFAO Motors.
credits: Lukaza
Post a Comment