Waziri
Mkuu Mizengo Pinda akipiga makofi mara baada ya kumkabidhi tuzo Mkurugenzi wa
Hifadhi za Taifa TANAPA Bw. Allan Kijazi anayenyanyua juu juu tuzo ya Mbuga ya
wanyama ya Serengeti mara baada ya kuitangaza mbuga hiyo kuwa ni moja ya maajabu
saba ya asili katika bara la Afrika kwenye hoteli ya Mount Meru, Kushoto ni Bw
Philip Imler Mwanzilishi wa Taasisi ya Seven Natural Wonders Bw. Philip
Imler.
Tanzania
imefanikiwa kushinda kupitia vivutio vyake vitatu vya utalii ambavyo ni Mlima
Kilimanjaro, Ngorongoro Crates na Mbuga ya wanyama ya Serengeti, hafla hiyo
imehudhuriwa na wageni waalikwa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mabalozi, Wafanya
biashara,Mawaziri, Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na wadau
mbalimbali wa utalii kutoka Mataifa mbalimbali katika ukanda wa Afrika
Mashariki.
Katika
picha kulia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki na Lynn
Imler mmja wa wakurugenzi wa Taasisi ya Seven Natural Wonders.
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda akimkabidhi zawadi ya picha ya Ngorongoro Crates muanzilishi
na muandaaji wa shindano la Seven Naturaral Wonders Bw.Phillip Imler mara baada
ya kumalizika kwa hafla ya kutangaza maajabu saba ya asili ya Afrika
iliyofanyika jana jioni kwenye Hoteli ya Mount Meru jijini
Arusha.
Vikundi
wa ngoma kutoka makabila ya mkoa wa Arusha vilipamba hafla hiyo
kamavinavyoonekana.
Wadau
kutoka TTB ambao pia walikuwa ni miongoni mwa wanakamati ya maandalizi wakiwa
katika picha ya pamoja
Mkurugenzi
wa Bodi ya Utalii TTB Dk. Aloyce Nzuki akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Iringa
mjini Mchungaji Msigwa, Kushoto ni Mh Shah kutoka Mafia na mmoja wa wajumbe wa
bodi ya Utalii TTB
Wabunge
wa bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzaniaakiwa katika hafla
hiyo.
Viongozi
mbalimbali wa dini walihudhuria pia.
Mbunge
Mh. James Lembeli akisalimiana na Bw. Mike Teyrol walipokutana katika hafla
hiyo.
Mwanamuziki
Mrisho Mpoto na Kundi lake wakitumbuiza wakati wa utoaji wa tuzo
hizo.
Mkurugenzi
wa Masoko wa Bodi ya Utalii Bi Devitha Mdachi akiwa pamoja na maafisa wengine wa
bodi hiyo wakipokea wageni mbalimbali waliofika katika hafla
hiyo.
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akizungumza
jambo na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Dk. Aloyce
Nzuki.
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akizungumza na
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi Maimuna Tarishi katikati ni msaidizi wake Bw.
Miskanji.
Kikundi
cha ngoma kikitumbuiza katika hafla hiyo.
Waziri
Mkuu akiwa meza kuu pamoja na viongozi wengine wakati wa utoaji wa tuzo hizo za
Seven Natural Wonders jijini Arusha jana jioni., kutoka kulia ni Magesa Mulongo
mkuu wa Mkoa wa Arusha, Agness Agunyu Waziri wa Utalii kutoka nchini Uganda na
kutoka kushoto ni Bw. Philip Imler kutoka Taasisi ya Seven Natural Wonders na
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki.
Mkurugenzi
wa Hifadhi za taifa TANAPA Bw. Allan Kijazi akiwasikiliza wabunge waliohudhuria
katika hafla hiyo kulia ni Deo Filikunjombe na kushoto ni David
Kafulila.
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda akiongozwa na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Dk. Aloyce Nzuki
wakati alipowasili kwenye hoteli ya Maount Meru kwa ajili ya utoaji tuzo
hizo.
Mama
Tunu Pinda wa pili kutoka kushoto akiwa katika hafla hiyo, kulia ni Mkurugenzi
wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Dk Aloyce Nzuki na katikati ni Lynn Imler
kutoka Seven Natural Wonders.
Mabalozi
mbalimbali waliohudhuria katika hafla hiyo wa kwanza kutoka kulia ni Balozi
Mutinda Mutiso Balozi wa Kenya Nchini Tanzania.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akizungumza na mbunge wa jimbo la
Arusha Mjini Bw. Godbless Lema kabla ya kuanza kwa hafla hiyo.
Mkurugenzi
wa Bodi ya Utalii nchini Tanzania (TTB) Dk. Aloyce Nzuki akiongea katika hafla
hiyo.
Bw Allan
Kijazi kushpto akiwa na wadau wengine katika hafla hiyo.
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda akimkabidhi tuzo ya Hifadhi ya Ngorongoro Crates Mkurugenzi
wa Hifadhi za Taifa TANAPA Bw. Allan Kijazi katika hafla hiyo, kushoto ni
Philip Imler wa Seven Natural Wonders.
Mkurugenzi
wa Hifadhi za Taifa TANAPA Bw. Allan Kijazi akiongea katika hafla
hiyo.
muanzilishi
na muandaaji wa shindano la Seven Naturaral Wonders Bw.Phillip Imler akizungumza
katika hafla hiyo.
Tuzo ya
mlima Kilimanjaro ikapokelewa na mhifadhi wa mlima huo kulia ni Waziri Mkuu
Mizengo Pinda na Philip Imler kushoto.
Balozi
Khamis Kagasheki ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii akizungumza katika
hafla hiyo iliyofanyika jana kwenye hoteli ya Mount Meru jijini
Arusha.
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika jana kwenye hoteli
ya Mount Meru jijini Arusha.
Balozi
wa Kenya nchini Tanzania akizungumza na Balozi Charles Sanga Mwenyekiti wa Bodi
ya Utalii nchini Tanzania TTB na Mkurugenzi wa bodi hiyo Dk. Aloyce Nzuki wakati
wa hafla hiyo.
**************************************
Na Mahmoud Ahmad,Arusha
TANZANIA
imepata tuzo tatu za maajabu saba ya Afrika kupitia vivutio vyake bora vya
utalii vya Mlima Kilimanjaro,Hifadhi ya Ngorongoro na Hifadhi ya Serengeti
ambayo ndio iliongoza kwa kupata kura nyingi kuliko nchi nyingine
yeyote.
Akitangaza
matokeo hayo jana mjini hapa rais wa taasisi iliyoandaa tuzo hiyo Dk. Phillip
Imler wa Marekani mbele ya waziri mkuu Mizengo Pinda alisema sababu iliyopelekea
Tanzania kupata ushindi huo ni kutokana na kuwa na vivutio vya
kipekee.
Akielezea
hifadhi ya taifa ya Serengeti alisema kuwa ndio hifadhi ya kipekee iliyopata
kura nyingi na kutokana na tabia za misafara ya wanyama wanaohama kwa msimu
maarufu kama annul animal migration.
Waziri Mkuu Mizengo
Pinda, aliyekuwa mgeni rasmi katika ghafla hiyo, alisema kuwa nchi za Afrika
zina vivutio vingi vya utalii na fursa kubwa ya kukuza pato kupitia utalii
huo.
Alisema
kutokana na sifa ambayo Tanzania imezipata kupitia vivutio vyake vitatu
itaendelea kuvitunza kuhakikisha kuwa vinavutia zaidi watalii na kuongeza pato
la taifa.
“Afrika
ina vivutio vingi vyenye kuvutia hivyo kila nchi ni lazima ijivunie rasilimali
hizo kwa kuvitunza na kuviendeleza,”alisema
“Kwa
Tanzania ni bahati ya pekee kwa kuweza kupata tuzo tatu za maajabu saba ya
Afrika ambazo ni za Mlima Kilimanjaro, Bonde la Ngorongoro pamoja na hifadhi ya
Taifa ya Serengeti hivyo ni wajibu wa kuvitunza na kuviendeleza,”alisema
Pinda.
Aliongezea
kuwa iwapo watanzania wataendeleza tabia ya utunzaji wa vivutio vilivyopo
nchini, nchi itaendelea kupata sifa duniani kote.
Naye
Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa,(TANAPA),Dkt. Alan Kijazi alisema mlima
Kilimanjaro ni mlima mrefu barani Afrika na hivyo una kila sababu ya kushinda na
watanzania waendelee kuutunza.
Dkt
Kijazi alisema kuwa hifadhi hiyo imeshinda kwa kuwa kuwa na wanyama wa kila aina
kama Big Seven, Simba, tembo, Viboko, Nyati, Vifaru, Sokwe na
Mamba.
Mbali na
Tanzania Dk.Imler alivitaja vivutio vingine vilivyoshinda kuwa ni Red sea Reefs,
Okavango Inland delta iliyopo nchini Botwasana, Sahara Desert na River
Nile.
Aidha
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki alisema ushindi huo ni
historia kubwa duniani na kwamba ni jambo la watanzania wote
kujivunia.
Pia
aliwashukuru wananchi walioshiriki katika mchakato mzima wa kupiga kura na
kuviwezesha kuingia katika ushindi kwa mara tatu.
Post a Comment