Polisi wakiwa wameimarisha ulinzi nje ya jengo la Sukari lililopo mkabala na Makutano ya Barabara za Ohio na Sokoine Driver Posta jijini Dar es salaam jengo hilo ndmo zilimo ofisi za mwendesha mashtaka wa Serikal Dk.Eliezer Feleshi, Ulinzi huo umeimarishwa kutokana na tishio la wafuasi wa Shekh Ponda kutishia kuandamana kwenda kwa Mwendesha Mashtaka huyokushinikiza Shekh Ponda aachiwe huru.
Baadhi ya wafuasi hao wa
Shekh Ponda wamekamatwa katika maeneo mbalimbali wakati wakijaribu kuingia
katika eneo la Posta ambapo ulinzi mkali uliimarishwa huku polisi wakitumia
Magari, Pikipiki, Mbwahuku makachero wakizunguka kila
mahali.
Baadhi ya Barabara
zilifungwa ili kuweka eneo hilo katika hali ya usalama zaidi na kuhakikisha
linzdhibitiwa na kulidwa kirahisi.
Askari Polisi wakifanya doria kwa
kutumia pikipiki kam wanavyoonekana wakiranda katika mitaa mbalimbali Posta
jijini Dar es salaam.
Baadhi ya waumini wa Dini ya Kiislamu
wakirushwa kichura leo Katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Dar es Salaam
walipokamatwa kwa tuhuma za kuandamana kushinikiza Sheikh Ponda aachiwe kwa
dhamana.
Askari Kanzu akiwa amemkamata muumini wa Dini
ya Kiislamu katika pilikapilika za kudhibiti maandamano ya kushinikiza Mahakama
imuachie kwa dhamana Katibu wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu, Sheikh Issa
Ponda, Dar es Salaam
Baadhi ya watuhumiwa wa maandamano hayo wakipandishwa kwenye gari la Polisi baada ya kukamatwa.
Mmoja wa maaskari wakifunga kamba
iliwaandamanaji wasiingie Makao Makuu ya jeshi hilo
Askari wa kudhibiti ujambazi wakiwa kwenye doria kusaidia kudhibiti maandamano
Baadhi ya watuhumiwa wa maandamano hayo wakipandishwa kwenye gari la Polisi baada ya kukamatwa.
Askari wa kudhibiti ujambazi wakiwa kwenye doria kusaidia kudhibiti maandamano
Wafuasi hao wa Shekh Ponda
wakipandishwa kwenye gari la polisi mara baada ya kukamatwa katika maandamano
hayo.
Post a Comment