Mkutubi msaidizi wa
Maktaba ya Watoto wenye ulemavu katika shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Joyce
Nyamuhokwa (katikat) akimwelezea Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji nchini
(TBC), Clement Mshana kuhusu maktaba hiyo wakati shirika hilo kwa kushirikiana
na kampuni ya magodoro ya Vita Foam (T) ltd walipokwenda kutoa msaada wa
magodoro 100 yenye thamani ya sh milioni 3, Dar es Salaam leo. Wengine ni Mkuu
wa Shule hiyo, Anna Mang’enya (wa pili kushoto), Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu
wa Vitafoam, Justine Mwakalinga (wa tatu kushoto) na wafanyakazi wengine wa Vita
Foam, TBC na walimu wa shule hiyo.
Shirika la Utangazaji
nchini (TBC) pamoja na Kampuni ya magodoro ya Vita Foam (T) Limited, leo
wamekabidhi msaada wa magodoro 100 yenye thamani ya shilingi Milioni 3 kwa Shule
ya Msingi ya Uhuru Mchanganyiko, Dar es Salaam. Msaada huo ni sehemu ya
marejesho ya faida inayoipata kwa jamii (CSR).
Akizungumza mara baada ya
kukabidhi msaada huo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC),
Clement Mshana amesema Jamii inayo wajibu wa kusaidia makundi ya watoto wenye
ulemavu nchini ili kuwapa faraja na wajione nao ni sehemu ya
jamii.




Post a Comment