Meneja wa Tigo Bw. William
Mpinga akielezea jinsi kampuni ya Tigo ilivyoshinda nafasi ya nane duniani yenye
mahusiano ya karibu na wateja wake kwenye mtandao wa kijamii wa
Facebook.
Tigo Tanzania imetajwa kuwa
miongoni mwa makampuni bora zaidi duniani yenye mahusiano ya karibu na wateja
wake kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook. Hii ni kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa na shirika la SocialBokers tarehe 7 February, 2013 ambalo lilifanya
utafiti wa makampuni 10 bora zaidi duniani yenye uhusiano wa karibu na wateja
kwenye mitandao ya jamii kwenye kipindi cha robo ya mwisho wa mwaka 2012. Tigo
Tanzania ndiyo shirika pekee la simu kutoka kanda ya Kati, Mashariki na Kusini
mwa bara la Afrika lililofikia viwango hivyo vilivyojumuisha makampuni yote bora
duniani.
Mitandao ya kijamii
inajitokeza kuwa njia rahisi zaidi kwa wateja mbali mbali kupata taarifa, kuomba
misaada na kuelimishwa kuhusu bidhaa mbalimbali, na makampuni yaliyo na
uhusiano bora na wateja wao na yenye uwezo mkubwa yamechukua fursa hii
kuboresha mahusiano na kuwa karibu na wateja wao. Mitandao hii mikubwa ya
kijamii duniani kama vile Facebook, hutoa njia m-badala na iliyo bora kwa
mashirika yaliyozidiwa ki-huduma na hivyo kutoa fursa kwa watu wa tamaduni mbali
mbali kushirikishana kujadili na kueleweshana.
” Tigo Tanzania imeibuka
kuwa namba 8 duniani kote kwenye tafiti hizi kutokana na kujikita vilivyo kwenye
kuhakikisha kuwa inatoa huduma bora na za kujitosheleza kwa wateja
wake.Tunathamini sana wateja wetu na tunahakikisha kuwa tuko pamoja nao wakati
wote kila wanapotuhijati. Maendeleo ya kiteknolojia na dijitali yamewezesha
kuwepo kwa mijadala mingi kila wakati kwenye mitandao ya kijamii. Tigo kama
Kinara wa uvumbuzi wa bidhaa za mawasiliano inatazama changamoto hii kama fursa
ya kujiweka karibu zaidi na wateja na kushirikiana nao kwa ukaribu zaidi. Kila
tunachofanya Tigo ni kwa ajili ya wateja wetu, hivyo kutambuliwa huku ki-dunia
ni fahari kubwa sana kwetu” alisema Ndg. William Mpinga Manager brand ya
Tigo.
Kwa mujibu wa shirika la
SocialBoker, utafiti wa mashirika yanayojituma zaidi kijamii kwa kipindi cha
mwezi Oktoba na Desemba, 2012, umeonyesha kuwa mashirika huwajibika na kujibu
hoja kutoka kwa wateja wao haraka zaidi kwenye kurasa za Facebook. Hoja
iliyokuwa inajibiwa kwa wastani wa masaa 21 miezi ya nyuma sasa makampuni
yanaweza kujibu kwa kipindi cha masaa 19.5 tu kuelekea mwishoni mwa 2012.
Shirika la simu la Tigo Tanzania limepata asilimia 87.30% kwa kujibu hoja ndani
ya masaa 28.
“Tigo Tanzania mbali ya
kujibu hoja za wateja kwenye mitandao ya kijamii inahakikisha kuwa inafanya
hivyo kwa ufanisi zaidi kila wakati. Kwa kuwa mstari wa mbele kwenye kutambua
hilo tumefanikiwa kupata heshima hii kubwa. Tutazidi kuongeza ubunifu ili
kuboresha huduma na bidhaa zetu, na tunatambua kwamba, ili kutoa huduma stahili,
ushiriki wa wateja wetu ni nyenzo muhimu sana. Tumepata mafanikio makubwa
tuliyonayo na kufika hapa tulipo leo kwa kuupa utoaji wa huduma bora kipaumbele,
na
kwa heshima hii kubwa,
tunaahidi kuwa tutajikita kuhakikisha tunaendelea kutoa ufumbuzi wa mawasiliano
uliobora zaidi jambo litakalomfanya kila mteja wetu kutabasamu.” alihitimisha
Ndg Diego Gutierrez, Managa wa Tigo.
Socialboker ndilo shirika
linaloongoza duniani miongoni mwa mashirika yanayofanya tafiti na kutoa takwimu
kuhusu mitandao ya kijamii ya Facebook, Twitter, Google+, LinkedIn na You tube.
Kwa njia hii inasaidia makampuni uwezo wa kampeni za kijamii za makampuni yao.
Tafiti za hivi karibuni zinajumuisha taarifa za Desemba 2012 za ‘Global Social
Media Report’ ambapo utafiti mkubwa ulifanywa ukihusisha idadi ya kurasa za
Facebook na watumiaji wake kidunia katika mataifa ya Marekani, Uingereza na
Brazili. Mengine ni Azerbaijan, Serbia, Mexico, Poland na El Salvador- kwa
kutaja machache
Post a Comment