IMEELEZWA kuwa ukosefu wa
utaalamu wa kutosha katika eneo la urejeshaji wa mali zilizopatikana kwa
njia haramu ndicho chanzo cha kumomonyoka kwa maadili na ongezeko la vitendo
vya makosa ya jinai katika jamii.
Hayo
yalisemwa leo (jana) na Mkurugenzi wa Mashtaka(wakati akifungua
mafunzo ya kuijengea nchi uwezo wa urejeshaji wa mali zilizopatikana kwa njia
haramu yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano wa jengo la Haki House, jijini
Dares Salaam.
“Wahalifu wamekuwa
kukiendelea kufanya vitendo hivi na kufahia matunda yake, kwa sababu wapelelezi
waendesha mashtaka na maofisa wa mahakama kutokuwa na utaalamu kwenye eneo la
urejeshaji wa mali zilizopatika kwa njia haramu. Ofisi yangu imewaalika
wataalamu kutoka World Bank/ StAR intiative kwa ajili ya kutoa ushauri na
mbinu za kuweza kukabiliana na changamoto hii,alisema
Feleshi.
Alisema maafunzo hayo
yamewashirikisha wadau mbalimbali kutoka Benki ya Kuu ya Tanzania (BOT),
Financial Interligent Unit,Polisi,Wizara ya Malia Asili, Usalama wa Taifa na
Wakala wa Usajili wa Leseni za Kampuni (BRELA).
Aidha Feleshi alisema
mafunzo hayo yatakamilika Februari 27, mwaka huu yatasaidia kuwapa wadau hao
uzoefu kutoka nchi ya Afrika Kusini, ambayo imeonekana kufanya vizuri. Pia
wadau hao watapata ujuzi jinsi taasisi hiyo inavyofanya kazi
.
Feleshi alisema mafunzo
hayo yatawasaidia wadau hao kuona namna ya kuweza kufanya kazi kwa pamoja ili
kudhibiti tatizo la wahalifu kufanya vitendo hivyo,lakini mali zao hazirejeshi
serikali au kwa wahusika.
Alisema
ofisi yake ilianzisha kitengo hicho mwaka 2009, imeshaanza kulifanyia kazi suala
hilo, hivyo mhalifu anapofanya uhalifu anachunguzwa na mali zake
huchunguzwa ili kuona zimepatikana vipi huku akitolea mfano wa meli ya uvuvi ya
Kichina ambayo ilitaifishwa na kurejesha
serikalini
Post a Comment