Wakuu wa nchi za Jumuiya
nchi za Kiislam(OIC) wakiwa katika picha ya pamoja, mara baada ya kumalizika kwa
kikao chao jijini Cairo, Alhamisi, Febr 7, 2013
Jumuiya ya nchi za Kiislamu Duniani (OIC) imezitaka
pande mbili zinazopigana nchini Syria (Upande wa serikali na waasi wa FSA)
kumaliza mapigano kwa njia ya majadiliano. Tangu kuanza kwa mapigano hayo mwezi
machi 2011,zaidi ya watu 60,000 wameripotiwa kuuawa. Serikali ya Syria iliyo
chini ya Rais Bashar Al Assad imekuwa ikizilaumu nchi za Magharibi na washirika
wao wa Saudi Arabia, Qatar na Uturuki kwa kuwapa waasi silaha na
fedha.
Post a Comment